Ratiba ya Mtihani wa Upimaji wa Darasa la Pili 2025, Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza rasmi Ratiba ya Mtihani wa Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Pili 2025.
Mtihani huu ni wa ngazi ya shule na unalenga kupima uwezo wa wanafunzi wa darasa la pili katika stadi tatu kuu za msingi ambazo ni kusoma, kuandika (Writing: Basic English Language Skills) na kuhesabu (Arithmetic Skills).
Upimaji huu ni hatua muhimu inayosaidia kutathmini kiwango cha uelewa na maendeleo ya wanafunzi katika umilisi wa somo la lugha na hisabati.
Ratiba ya Mtihani wa Upimaji wa Darasa la Pili 2025
Mtihani wa Upimaji wa Darasa la Pili 2025 umepangwa kuanza kufanyika mwezi Novemba 2025 kama ifuatavyo:
Tarehe | Siku | Muda | Somo/Stadi |
18/11/2025 | Jumanne | 2:00 – 2:40 | Kuandika: Basic English Language Skills |
2:40 – 3:40 | Mapumziko | ||
3:40 – 4:30 | Stadi ya Kuhesabu (Arithmetic Skills) | ||
19/11/2025 | Jumatano | 2:00 – 5:00 | Stadi ya Kusoma |
20/11/2025 | Alhamisi | – | (Kwa shule zenye zaidi ya wanafunzi 300, stadi ya kusoma inaweza kuendelea siku hii) |