Majina ya Waliochaguliwa Vyuo Vya Kati 2025/2026, Wahitimu wengi wa elimu ya sekondari ngazi ya kidato cha nne nchini Tanzania huwa na ndoto mbalimbali kuhusu mustakabali wa maisha yao baada ya mitihani ya taifa.
Ili kutambua na kukuza ndoto hizi, Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Ofisi ya Rais – TAMISEMI, imeweka njia mbalimbali zinazomsaidia mwanafunzi kuchagua mwelekeo wa maisha yake ya kitaaluma kulingana na uwezo na matamanio aliyo nayo.
Njia hizi mbili kuu ni kuendelea na elimu ya kidato cha tano au kujiunga na vyuo vya kati. Wakati baadhi ya wanafunzi wanachagua njia ya kidato cha tano kwa lengo la kufikia elimu ya juu na shahada, si wote wanaofaulu kupata alama zinazokidhi vigezo vya kuchaguliwa.
Hapo ndipo umuhimu wa vyuo vya kati unapojitokeza—njia mbadala yenye nafasi pana, isiyohitaji ufaulu wa hali ya juu kulinganisha na njia ya kidato cha Tano lakini inayoandaa wataalamu wa fani mbalimbali kwa soko la ajira la ndani na nje ya nchi.
Majina ya Waliochaguliwa Vyuo Vya Kati 2025/2026 (Selection Vyuo Vya Kati)
Ni Lini Majina ya Waliochaguliwa Vyuo Vya Kati 2025/2026 Yatatangazwa?
Baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kutangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne, Ofisi ya Rais – TAMISEMI huanza mchakato wa upangaji wa wanafunzi katika shule na vyuo.
Kwa kawaida, orodha ya majina ya waliochaguliwa vyuo vya kati 2025/2026 hutangazwa rasmi kuanzia mwezi Juni 2025, ikifuatiwa na mizunguko mingine ya uteuzi kama itahitajika.
Ni muhimu kwa wanafunzi na wazazi kufuatilia tovuti rasmi ya TAMISEMI ili kupata taarifa za haraka na sahihi kuhusu uchaguzi huu.
Jinsi ya Kuangalia Majina ya Waliochaguliwa Vyuo vya Kati 2025/2026
Ili kuona kama umechaguliwa kujiunga na chuo cha kati kwa mwaka wa masomo 2025/2026, fuata hatua hizi:
- Tembelea tovuti rasmi ya TAMISEMI kupitia kiungo: https://selform.tamisemi.go.tz
- Bofya kipengele cha “Selection Results”
- Chagua mkoa na wilaya ulipofanya mtihani wa kidato cha nne.
- Tafuta jina la shule yako ya sekondari na uangalie majina ya wanafunzi waliochaguliwa kutoka shule hiyo.
- Tafuta jina lako kwenye orodha na ujue chuo pamoja na kozi uliyopangiwa.
Orodha ya Majina ya Waliochaguliwa Vyuo vya Kati kwa Kila Mkoa 2025/2026
Ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa kwa wanafunzi na wazazi, tumeandaa jedwali lifuatalo likiwa na majina ya mikoa yote ya Tanzania Bara. Bonyeza jina la mkoa ili kufunguka ukurasa wenye wilaya zake na hatimaye kuona majina ya waliochaguliwa vyuo vya kati kwa mwaka wa masomo 2025/2026:
Kumbuka: Kiungo cha kila mkoa kitakupeleka moja kwa moja kwenye ukurasa wa TAMISEMI wenye orodha ya wilaya za mkoa huo mara baada ya majina hayo kutangazwa. Bonyeza jina la wilaya yako ili kuona wanafunzi waliopangiwa vyuo vya kati.
Serikali hutumia vigezo maalum kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaochaguliwa kwenda vyuo vya kati wanakidhi mahitaji ya kozi husika. Baadhi ya vigezo hivyo ni:
- Ufaulu wa jumla katika masomo ya kidato cha nne – hasa kwa masomo yanayohusiana na kozi aliyoomba mwanafunzi.
- Chaguo la mwanafunzi alipokuwa anajaza fomu ya Selform.
- Upatikanaji wa nafasi katika chuo na kozi husika.
- Uwiano wa kijinsia na muktadha wa kijiografia kwa kuzingatia usawa wa fursa.
Nini Kinafuata Baada ya Kuchaguliwa?
Mwanafunzi akishajua chuo alichopangiwa, anapaswa:
- Kupakua na kuchapisha barua ya kupokelewa chuoni ambayo hujulikana kama (Joining Instruction).
- Kujiandaa na mahitaji muhimu ya chuo kama ada, vifaa vya masomo, na makazi.
- Kuhakikisha anaripoti chuoni kwa tarehe iliyopangwa rasmi na TAMISEMI au uongozi wa chuo husika.