Nauli ya Basi Dar Es Salaam kwenda Dodoma, Safari ya basi kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma ni moja kati ya safari zenye idadi kubwa ya wasafiri kutokana na shughuli nyingi za kijamii na kiuchumi zinazoendelea baina ya mikoa hii miwili muhimu.
Safari hii, ambayo huchukua takribani masaa saba hadi kumi kutegemeana na aina ya basi na hali ya barabara. Safari ya kutoka dar es salaam kuelekea makao makuu ya nchi inahudumiwa na makampuni mbalimbali ya usafiri yanayotoa huduma za usafiri wa basi.
Miongoni mwa makampuni maarufu yanayo toa huduma ya kusafirisha abiria kutoka dar es salaam kwenda Dodoma ni Happy nation, Shabby, Abbood Bus, New force, Kimbinyiko n.k. Makampuni haya yamekua yakitoza nauli kulingana na viwango vilivyopangwa na LATRA (Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini).
Nauli ya Basi Dar Es Salaam kwenda Dodoma
Hadi hii leo May 2024, nauli za mabasi kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma zimewekwa kama ifuatavyo kulingana na aina ya basi na mamlaka husika (LATRA):
Aina ya Basi | Nauli (Tsh) | Umbali (km) |
Basi la kawaida (Ordinary) | 21000 | 424 |
Basi la kifahari (Luxury) | 29000 | 424 |
Tafadhali kumbuka kwamba nauli hizi zinaweza kubadilika kidogo kulingana na kampuni ya basi unayochagua kusafiri nayo. Baadhi ya kampuni huenda zikatoza kiasi kidogo zaidi au kidogo chini ya bei hizi elekezi za kawaida.
Ili kupata taarifa ya uhakika zaidi kuhusu nauli za mabasi, tunashauri uwasiliane moja kwa moja na kampuni ya basi unayotaka kusafiri nayo au kutembelea tovuti yao rasmi. Unaweza kununua tiketi yako moja kwa moja kwenye vituo vya mabasi au kupitia tovuti za kampuni za mabasi husika. Inashauriwa kununua tiketi mapema, hasa wakati wa misimu ya kusafiri yenye wasafiri wengi, ili kuepuka usumbufu wowote.