Jinsi Ya Kufahamu Bidhaa Feki Kwenye Biashara

WhatsApp Group Join Now
Telegram Group Join Now
Jinsi Ya Kufahamu Bidhaa Feki Kwenye Biashara, Mara nyingi tunanunua vitu na bidhaa mbalimbali Tanzania bila kuzifahamu au kuzichunguza vyema Hili limepelekea watu wengi kununua bidhaa zisizofaa kwao au zenye madhara kwenye afya zao.

Kutokana na ukosefu wa elimu pamoja na kuishi kwa mazoea, watu wengi hawajui wala hawachunguzi vyema bidhaa wanazozinunua ili kuhakikisha ubora wake.

Madhara ya kutumia bidhaa Fake au bandia:

  • Matatizo ya kiafya kama vile saratani na ulemavu.
  • Upotevu wa fedha.
  • Ajali (Milipuko au shoti ya umeme).
  • Huathiri uchumi.

Ni wazi kuwa yapo madhara mengi yatokanayo na matumizi ya bidhaa feki.

Jinsi Ya Kufahamu Bidhaa Feki Kwenye Biashara 

Hivyo ni vyema ukafahamu njia za kubaini bidhaa hizi.

SOMA HII  Ijue Elimu Ya Pesa Na Mafanikio

1. Bidhaa Fake Huwa na Matangazo Yasiyo Ya Kawaida

Wahenga walisema “Chema chajiuza kibaya chajitembeza”; ni vyema ukawa makini na bidhaa zenye punguzo kubwa la bei kuliko kawaida, kwani mara nyingi bei hupungua sana kutokana na ubora duni.

Pia ni vyema ukaepuka kuvutiwa na maneno ya kibiashara kama vile “Oringinal” Colection”, “King size”, “Royal”, “genuine,” “real,”, “authentic”, “Mpya” au “Kali”.

Kumbuka simaanishi usinunue bidhaa yenye punguzo au maneno haya bali yasiwe ndiyo yanatawala au kutumiwa kama mbinu ya mauzo.

2. Jitahidi Fahamu Bidhaa Yako

Ni vyema ukaichunguza na kuifahamu bidhaa ambayo unainunua au kuitumia mara kwa mara.

Hili litakuwezesha kubaini bidhaa ambayo ni Fake au bandia kwa urahisi zaidi.

Chunguza na bainisha vitu vya msingi ambavyo ni lazima viwepo kwenye bidhaa husika.

Hivyo kabla ya kununua bidhaa hakikisha inafanana na ile uliyoizoea.

kama hujawahi kuinunua unaweza kumwomba mtu anayeifahamu vyema akusaidie kuikagua.

3. Jitahidi Kukagua Vifungashio Kwa Makini

Kubaini bidhaa Fake au bandia kunahitaji utulivu, chukua muda kukagua vifungashio vya bidhaa husika kwa makini.

SOMA HII  App za Mikopo ya Haraka Tanzania

Hili litakuwezesha kubaini kukosekana kwa taarifa muhimu kama vile jina la mtengenezaji, mahali pa utengenezaji, tarehe ya kuzalishwa na ya mwisho wa matumizi pamoja na taarifa nyingine muhimu.

Bidhaa iliyokosa taarifa muhimu inaweza kuwa bandia au yenye ubora duni.

4. Jitahidi Kuhakikisha Kila Kilichotakiwa Kuwepo Kipo

Mara nyingi unaweza kununua kifaa au bidhaa yenye kitu zaidi ya kimoja Kwa mfano, ikiwa unanunua simu au kamera hakikisha kama huwa inauzwa pamoja na vifaa kama vile betri, chaja, memory card na waya wa USB vipo vyote tena kwenye hali nzuri.

Mara nyingi bidhaa feki hukosa badhi ya vifaa muhimu ambavyo kwa kawaida huwepo kwenye vifaa au bidhaa halisi.

5. Jitahidi Kuuliza Kuhusu Warranty

Warranty ni mkataba maalumu baina ya mnunuzi na mtengenezaji wa bidhaa husika.

Warranty hukuwezesha kutengenezewa au kubadilishiwa bidhaa husika ikiwa itapata matatizo ndani ya muda fulani.

Bidhaa bandia au feki kamwe huwa hazitoi Warranty na zikitoa basi ni Fake pia.

SOMA HII  Njia za Kufanikiwa Kiuchumi Tanzania

Hivyo ni vyema ukatazama kama bidhaa husika (Hasa vifaa vya kielektroniki) zina Warranty ya uhakika.

6. Jitahidi Kutembelea Tovuti Ya Mzalishaji

Hivi sasa karibu kila kampuni imejitahidi kufungua tovuti kwa ajili ya kuwafikia wateja wake kwa urahisi zaidi.

Pia kampuni nyingi zimekuwa zikijitahidi kuwawezesha wateja wake kubaini bidhaa feki.

Wakati mwingine, baadhi ya bidhaa huwekwa namba ambazo unaweza kuziingiza kwenye tovuti yao na kuona kama bidhaa ni bandia au laa.

Hivyo, unaweza pia kutumia njia hii ili kubaini na kuepuka bidhaa Fake.

7. Jitahidi Kununua Kutoka Kwa Wakala Aliyeidhinishwa

Ili kurahisisha na kuhakikisha ubora wa huduma, kampuni nyingi zimekuwa zikisajili mawakala kwenye maeneo mbalimbali.

Unaponunua bidhaa kutoka kwa wakala aliyeidhinishwa, ni rahisi zaidi kupata bidhaa halisi; pia upatapo tatizo utapata msaada kwa urahisi zaidi.

Kwa mfano, ikiwa unataka kununua simu ya Nokia au Sumsung, basi tafuta wakala aliyeidhinishwa na Nokia au Sumsung katika eneo lako.

8. Jitahidi Kuepuka Bidhaa Copy

Hivi leo unaweza kuona simu inayoitwa NOKLA, lakini ukiitazama kila kitu kinafanana na simu ya NOKIA N97.

Kwanini kama watengenezaji wa simu hii wanalengo zuri wasibuni muundo wao wenyewe? Ni dhahiri kuwa wanataka kuwadanganya na kuwachanganya wanunuzi huko kubadili jina na kuiita NOKLA ni mbinu tu ya kukwepa mkono wa sheria.

Ni wazi kuwa bidhaa hizi ni feki, hivyo yakupasa kuziepuka.

Hot this week

Nafasi za Kazi Jeshi la Magereza 2025

Jeshi la Magereza limetangaza nafasi mpya za ajira kwa...

Namna Ya Kuangalia Taarifa Za Usajili NIDA | Hatua kwa hatua

Namna Ya Kuangalia Taarifa Za Usajili NIDA, Kuangalia taarifa...

Mfumo wa Maombi ya Ajira kwa Walimu Mtandaoni (OTEAS)

Mwongozo wa Mfumo wa Maombi ya Ajira kwa Walimu...

Orodha ya Vifurushi vya Azam TV na Bei zake – Chagua Kifurushi Kinachokufaa

Azam TV imekuwa sehemu muhimu ya burudani ndani ya...

Sample/Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Jeshi la Magereza

Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Jeshi la...

Orodha ya Vifurushi vya Azam TV na Bei zake – Chagua Kifurushi Kinachokufaa

Azam TV imekuwa sehemu muhimu ya burudani ndani ya...

Jinsi ya Kupata Pesa kwa Biashara Ya Upigaji wa Picha Tanzania

Jinsi ya Kupata Pesa kwa Biashara Ya Upigaji wa...

Biashara Ndogo Ndogo Zenye Mtaji Kidogo

Biashara Ndogo Ndogo Zenye Mtaji Kidogo, Biashara ndogondogo zenye...

Jinsi ya kuandaa Tangazo La biashara kwa urahisi

Jinsi ya kuandaa Tangazo La biashara kwa urahisi, Kuandaa...

Bei Mpya Vifurushi vya Azam TV | Gharama Mpya za Vifurushi vya Azam TV

Bei Mpya Vifurushi vya Azam TV, Azam TV imekuwa...

Jinsi Ya Kulipia Vifurushi Vya Startimes

Startimes ni moja ya kampuni kubwa za utoaji huduma...

Related Articles

Popular Categories

Njia Rahisi ya Kuangalia Namba ya NIDA Kwa SMS

Njia Rahisi ya Kuangalia Namba ya NIDA Kwa SMS, Kupata namba ya NIDA kwa njia ya SMS ni rahisi na haraka. Njia hii ni...

Jinsi ya Kupata Mtoto wa Kiume

Jinsi ya Kupata Mtoto wa Kiume, Ni shauku ya kila mzazi kupata Watoto wa Jinsia tofauti katika uzao wao ingawaje Wengi hupata watoto wa...

Jinsi ya Kukopa Muda wa Maongezi Halotel | Menu ya kukopa Salio Halotel

Jinsi ya Kukopa Muda wa Maongezi Halotel, Je Unatumia mtandao wa simu wa halotel na umekwama na hujui hatua ,sifa na vigezo za kupata...