Wasifu CV ya Romain Folz Kocha Mpya wa Yanga 2025/2026

WhatsApp Group Join Now
Telegram Group Join Now

Wasifu CV ya Romain Folz Kocha Mpya wa Yanga 2025/2026, Kocha huyo ni Romain Folz, raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 35, anayekuja kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Miloud Hamdi aliyeondoka kuelekea Ismaily ya Misri.

Romain Folz, ambaye ana leseni ya kiwango cha juu ya UEFA Pro Licence pamoja na Pro Licence ya CONMEBOL, anachukuliwa kama mmoja wa makocha chipukizi wanaopanda kwa kasi barani Afrika, akiwa na uzoefu mkubwa katika kuvinoa vikosi vya timu mbalimbali za klabu na taifa katika bara la Afrika na nje ya Afrika.

Wasifu CV ya Romain Folz Kocha Mpya wa Yanga 2025/2026

Taarifa Maelezo
Jina kamili Romain Folz
Tarehe ya Kuzaliwa / Umri Juni 28, 1990 (Miaka 35)
Mahali alipozaliwa Bordeaux, Ufaransa 🇫🇷
Uraia Ufaransa 🇫🇷
Wastani wa muda kama kocha Miezi 4.5 (0.38 Miaka)
Leseni ya Ukocha UEFA Pro Licence
Mfumo anaoupenda 4-3-3 (Defending)
SOMA HII  Droo ya Klabu Bingwa Afrika 2025/2026 CAF Champions League

Cv ya Romain Folz Kocha Mpya wa Yanga 2025/2026

Historia na Uzoefu wa Ukocha: Folz na Safari ya Soka Afrika

Licha ya kuwa na umri mdogo, Romain Folz ana uzoefu mpana wa soka la Afrika, akiwa amefundisha vilabu kutoka nchi zaidi ya tano barani humo. Anafahamika kwa falsafa yake ya kiufundi inayojikita kwenye mfumo wa 4-3-3 unaohimiza pressing ya hali ya juu na uchezaji wa kushambulia.

Muhtasari wa Safari yake ya Kikazi:

  • 2025 – Mkurugenzi wa Michezo, Olympique Akbou – Algeria 🇩🇿
  • 2024 – Kocha Msaidizi, Mamelodi Sundowns – Afrika Kusini 🇿🇦
  • 2023 – Kocha Mkuu, Horoya AC – Guinea 🇬🇳
  • 2022–2023 – Kocha Mkuu, AmaZulu FC – Afrika Kusini 🇿🇦
  • 2021 – Kocha Mkuu, Township Rollers – Botswana 🇧🇼
  • 2021 – Kocha Mkuu, Ashanti Gold – Ghana 🇬🇭
  • 2020 – Kocha Mkuu, Bechem United – Ghana 🇬🇭
  • 2019 – Kocha Msaidizi, Pyramids FC – Misri 🇪🇬
  • 2019 – Kocha Msaidizi, Timu ya Taifa ya Uganda 🇺🇬
  • 2018 – Kocha Mkuu, West Virginia United – Marekani 🇺🇸
  • 2020–2021 – Kocha Msaidizi, Chamois Niortais FC – Ufaransa 🇫🇷
SOMA HII  Ratiba ya Azam FC Ligi Kuu Tanzania Bara 2025/26 NBC Premier League

Kocha Folz pia ni mshika vyeti vya juu kabisa vya ukocha duniani, akiwa na UEFA Pro Licence pamoja na CONMEBOL Pro Licence, jambo linaloonesha umahiri wake wa kitaalamu.

Mafanikio na Majukumu Yanayomkabili Yanga SC

Kuajiriwa kwa Romain Folz kunakuja wakati ambapo Yanga SC ina malengo makubwa zaidi kwa msimu wa 2025/2026, ikiwa ni pamoja na kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania, Ngao ya Jamii 2025, pamoja na kuendelea kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Majukumu yake ya awali yatakuwa:

  1. Kuiongoza Yanga kutwaa Ngao ya Jamii 2025
  2. Kufanikisha ushiriki wa Yanga katika Hatua ya Makundi ya CAF Champions League 2025/2026
  3. Kutetea mataji ya Kombe la Muungano na Kombe la FA yaliyopatikana msimu wa 2024/2025
SOMA HII  Timu 12 Zitakazoshiriki Mashindano ya CECAFA Kagame Cup 2025

Kwa rekodi na weledi wake, Romain Folz anatarajiwa kuleta mabadiliko chanya kwenye kikosi cha Yanga, si tu kwa kiwango cha mchezo uwanjani bali pia kwa mtazamo wa kisasa wa kiufundi.

Mbinu na Mtindo wa Uchezaji wa Romain Folz

Romain Folz anajulikana kwa kupendelea mfumo wa kisasa wa 4-3-3, unaohimiza pressing kali, pasi za haraka, na uwiano bora kati ya ulinzi na mashambulizi. Mtindo huu umemuwezesha kupata mafanikio katika vilabu mbalimbali barani Afrika, hususan akiwa na AmaZulu na Township Rollers.

Hot this week

Nafasi za Kazi Jeshi la Magereza 2025

Jeshi la Magereza limetangaza nafasi mpya za ajira kwa...

Namna Ya Kuangalia Taarifa Za Usajili NIDA | Hatua kwa hatua

Namna Ya Kuangalia Taarifa Za Usajili NIDA, Kuangalia taarifa...

Mfumo wa Maombi ya Ajira kwa Walimu Mtandaoni (OTEAS)

Mwongozo wa Mfumo wa Maombi ya Ajira kwa Walimu...

Orodha ya Vifurushi vya Azam TV na Bei zake – Chagua Kifurushi Kinachokufaa

Azam TV imekuwa sehemu muhimu ya burudani ndani ya...

Sample/Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Jeshi la Magereza

Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Jeshi la...

Wasifu CV ya Neo Maema Kiungo Mpya wa Simba 2025/2026

Klabu ya Simba SC imethibitisha kukamilisha usajili wa kiungo...

Wasifu CV Ya Mohamed Doumbia Kiungo Mpya wa Yanga 2025/2026

Mu Ivory Coast, Mohamed Doumbia (26) ametambulishwa na timu...

Ratiba ya Klabu Bingwa Afrika 2025/2026 Hatua ya Awali

Droo ya mashindano ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF)...

Timu 12 Zitakazoshiriki Mashindano ya CECAFA Kagame Cup 2025

Timu 12 Zitakazoshiriki Mashindano ya CECAFA Kagame Cup 2025 Timu...

Orodha ya Wafungaji Bora CHAN 2025

Orodha ya Wafungaji Bora CHAN 2025, Michuano ya CHAN...

Kikosi cha Taifa Stars vs Morocco Leo 22 August 2025 CHAN

Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ itacheza mchezo...

Wasifu CV Ya Rushine De Reuck Beki Mpya wa Simba 2025/2026

Klabu ya Simba imemtambulisha rasmi beki wa kati, Rushine...

Related Articles

Popular Categories

Njia Rahisi ya Kuangalia Namba ya NIDA Kwa SMS

Njia Rahisi ya Kuangalia Namba ya NIDA Kwa SMS, Kupata namba ya NIDA kwa njia ya SMS ni rahisi na haraka. Njia hii ni...

Jinsi ya Kupata Mtoto wa Kiume

Jinsi ya Kupata Mtoto wa Kiume, Ni shauku ya kila mzazi kupata Watoto wa Jinsia tofauti katika uzao wao ingawaje Wengi hupata watoto wa...

Jinsi ya Kukopa Muda wa Maongezi Halotel | Menu ya kukopa Salio Halotel

Jinsi ya Kukopa Muda wa Maongezi Halotel, Je Unatumia mtandao wa simu wa halotel na umekwama na hujui hatua ,sifa na vigezo za kupata...