Bei ya Tiketi za Treni Ya Mwendokasi SGR, Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imetangaza rasmi nauli za safari za treni ya mwendokasi ya SGR, na habari njema kwa wasafiri wote nchini ni kwamba bei za nauli sio kubwa kama wengi walivotarajia.
Na kwa familia zinazosafiri na watoto wadogo, kuna habari njema zaidi: watoto chini ya miaka minne watasafiri bure kabisa!
LATRA imeweka nauli hizi kwa kuzingatia umbali wa safari, hivyo kuhakikisha kuwa wasafiri wanalipa kiwango cha haki kulingana na umbali wanaosafiri. Nauli hizi zina ushindani mkubwa ukilinganisha na mabasi yaendayo Dodoma, ambayo kwa kawaida hutoza kati ya Tsh 29,000 na Tsh 35,000. Kwa hivyo, SGR haitoi tu safari ya haraka na ya starehe bali pia ni chaguo la kiuchumi kwa wasafiri wengi.
Bei ya Tiketi za Treni Ya Mwendokasi SGR
Nauli za Treni ya mwendokasi zimewekwa kwa kuzingatia umbali wa safari usika na umri wa abiria. Kwa watu wazima na watoto wenye umri zaidi ya miaka 12, bei ya tiketi imetajwa kuwa ni Tsh. 69.51 kwa kila kilomita. Watoto wenye umri kati ya miaka 4 na 12 watalipa nusu ya bei hiyo, yaani Tsh. 34.76 kwa kilomita. Watoto chini ya miaka minne watasafiri bure, lakini taarifa zao zitahitajika kurekodiwa.
Bei ya Tiketi Treni ya Mwendokasi SGR Kwa Abiria Wenye umri zaidi ya miaka 12
Bei ya Tiketi za Treni Ya Mwendokasi kwa daraja la kawaida kulingana na umbali wa vituo kuanzia Dar es Salaam hadi Makutupora kwa watu wazima na watoto wenye umri zaidi ya miaka 12 ni kama ifuatavyo;
Safari | Umbali (Km) | Nauli (Shilingi) | |
Kutoka | Kwenda | Daraja la Kawaida | |
Dar es Salaam | Pugu | 19 | 1000 |
Dar es Salaam | Soga | 51 | 4000 |
Dar es Salaam | Ruvu | 73 | 5000 |
Dar es Salaam | Ngerengere | 134.5 | 9000 |
Dar es Salaam | Morogoro | 192 | 13000 |
Dar es Salaam | Mkata | 229 | 16000 |
Dar es Salaam | Kilosa | 265 | 18000 |
Dar es Salaam | Kidete | 312 | 22000 |
Dar es Salaam | Gulwe | 354.7 | 25000 |
Dar es Salaam | Igandu | 387.5 | 27000 |
Dar es Salaam | Dodoma | 444 | 31000 |
Dar es Salaam | Bahi | 501.6 | 35000 |
Dar es Salaam | Makutupora | 531 | 37000 |
Bei Ya Tiketi Kwa Abiria Wenye umri Kuanzaia Miaka 4 hadi 12
Aidha, mchanganuo wa Bei ya tiketi za Treni ya mwendokasi kwa daraja la kawaida kulingana na umbali wa vituo kuanzia Dar es Salaam hadi Makutupora kwa watoto wenye umri kuanzia miaka minne (4) hadi 12 ni kama ifuatavyo;
Safari | Umbali (Km) | Nauli (Shilingi) | |
Kutoka | Kwenda | Daraja la Kawaida | |
Dar es Salaam | Pugu | 19 | 500 |
Dar es Salaam | Soga | 51 | 2000 |
Dar es Salaam | Ruvu | 73 | 2500 |
Dar es Salaam | Ngerengere | 134.5 | 4500 |
Dar es Salaam | Morogoro | 192 | 6500 |
Dar es Salaam | Mkata | 229 | 8000 |
Dar es Salaam | Kilosa | 265 | 9000 |
Dar es Salaam | Kidete | 312 | 11000 |
Dar es Salaam | Gulwe | 354.7 | 12500 |
Dar es Salaam | Igandu | 387.5 | 13500 |
Dar es Salaam | Dodoma | 444 | 15500 |
Dar es Salaam | Bahi | 501.6 | 17500 |
Dar es Salaam | Makutupora | 531 | 18500 |
Uchambuzi
- Nauli ya Standard Class ya kawaida iko kwa wastani wa TSh 13,000 kwa mtu mzima—hii ni chaguo rahisi na nafuu kwa wengi.
- Kama unatafuta haraka zaidi na huduma zaidi, Express ni bora—bei kati ya TSh 20,000–22,000.
- Kwa familia, watoto wa umri wa miaka 4–12 wanapata punguzo la 50%, na chini ya miaka 4 wanapanda bure.
Mapendekezo
- Kwa bei nafuu na haraka: chagua Standard Class (TSh 13,000).
- Kwa haraka zaidi (Express): angalia chaguo za TSh 20–22,000, ikiwa unaona thamani kwa muda uliookolewa.
- Kwa familia: hakikisha umepata taarifa lazima kuhusu punguzo kwa watoto (4–12) na usafiri wa bure kwa chini ya miaka 4.
Bei rasmi ya Standard Class Dar es Salaam → Morogoro inakadiriwa kuwa karibu TSh 13,000 kwa mtu mzima; bei za Express zinaweza kufikia TSh 20,000–22,000, kulingana na aina ya daraja. Watoto 4–12 wanapata nusu ya bei, na chini ya 4 wasafiri kwa bure.