Bei Ya Unit Moja Ya Umeme Tanzania – TANESCO

WhatsApp Group Join Now
Telegram Group Join Now

Bei Ya Unit Moja Ya Umeme Tanzania, Umeme ni aina ya nishati muhimu sana katima maisha ya kilasiku na inatumika kwa shughuli mbalimbali. Kwa miaka kadhaa iliyopita, umeme haukuwa na umuhimu kama ulivyo sasa.

Kwa mfano, vituo vya afya vitapata shida kutoa huduma bora bila umeme wa kuendesha vifaa vya matibabu. Vilevile, viwanda na biashara vitakumbana na changamoto kubwa katika shughuli zao bila usambazaji wa umeme wa uhakika.

Bei Ya Unit Moja Ya Umeme Tanzania 

Umeme ni sehemu muhimu ya jamii ya kisasa, na hutumiwa kuendesha nyumba zetu na biashara. Nchini Tanzania, gharama ya unit moja ya umeme inaweza kutofautiana kulingana na mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na jiografia, chanzo cha nishati, na sera za serikali. Katika makala hii, tutatoa muhtasari wa bei ya umeme nchini Tanzania

SOMA HII  Dira Ya Mafanikio Tanzania

Bei za Umeme kwa Makundi Mbalimbali ya Wateja (Unit Moja ya Umeme Shilingi Ngapi)

Kwa mujibu wa Sheria ya EWURA, Sura ya 414, na Sheria ya Umeme, Sura ya 131, bei za umeme nchini Tanzania zimeidhinishwa na EWURA na ni kama ifuatavyo:

Bei za Umeme kwa Makundi Mbalimbali ya Wateja

D1: Wateja wa Majumbani

  • Bei ya Nishati (0 – 75 kWh): TZS 100 kwa kWh
  • Bei ya Nishati (Zaidi ya 75 kWh): TZS 350 kwa kWh

Wateja hawa ni wale wanaotumia wastani wa unit 75 kwa mwezi. Matumizi yatakayozidi unit 75 yatatozwa bei ya juu ya TZS 350 kwa kila unit inayozidi. Umeme unatolewa katika msongo mdogo wa umeme kwenye njia moja (230V).

SOMA HII  Makato ya kutuma Pesa NMB kwenda CRDB

T1: Wateja wa Kawaida

  • Bei ya Nishati: TZS 292 kwa kWh

Wateja hawa ni pamoja na wateja wa majumbani, biashara ndogondogo, viwanda vidogo, taa za barabarani, na mabango. Umeme unatolewa katika msongo mdogo wa umeme kwenye njia moja (230V) na njia tatu (400V).

T2: Wateja wa Matumizi Makubwa

  • Bei ya Nishati: TZS 195 kwa kWh
  • Tozo ya Huduma: TZS 14,233 kwa mwezi
  • Bei ya Mahitaji ya Juu: TZS 15,004 kwa kVA/Mwezi

Wateja hawa ni wale wenye matumizi ya kawaida ya umeme kupitia 400V na matumizi kwa mwezi ni zaidi ya unit 7,500.

T3-MV: Wateja wa Msongo wa Kati

  • Bei ya Nishati: TZS 157 kwa kWh
  • Tozo ya Huduma: TZS 16,769 kwa mwezi
  • Bei ya Mahitaji ya Juu: TZS 13,200 kwa kVA/Mwezi
SOMA HII  Biashara Ndogo Ndogo Zenye Mtaji Kidogo

Wateja hawa wameunganishwa katika msongo wa kati wa umeme (Medium Voltage).

T3-HV: Wateja wa Msongo Mkubwa

  • Bei ya Nishati: TZS 152 kwa kWh
  • Bei ya Mahitaji ya Juu: TZS 16,550 kwa kVA/Mwezi

Wateja hawa ni pamoja na ZECO, Bulyanhulu, na Twiga Cement, ambao wameunganishwa katika msongo mkubwa wa umeme (High Voltage).

Umeme wa 5000 ni Unit Ngapi?

Ili kuelewa vizuri jinsi bei ya umeme inavyopimwa, ni muhimu kujua umeme wa kiasi fulani wa fedha ni sawa na unit ngapi.

Kwa mfano, kwa wateja wa kundi la D1, umeme wa TZS 5000 unaweza kua unit 50 ikiwa matumizi ya mteja yapo chini ya unit 75. Ikiwa matumizi ya mteja yanazidi unit 75, bei itakuwa TZS 350 kwa kWh kwa units zinazozidi.

Umeme wa 1000 ni Unit Ngapi?

Kwa wateja wa kundi la D1, umeme wa TZS 1000 unaweza kutoa unit 10 kwa matumizi ya chini ya unit 75. Ikiwa matumizi ya mteja yanazidi unit 75, basi TZS 1000 itakuwa sawa na takribani unit 2.86 kwa bei ya TZS 350 kwa kWh.

Hot this week

Nafasi za Kazi Jeshi la Magereza 2025

Jeshi la Magereza limetangaza nafasi mpya za ajira kwa...

Namna Ya Kuangalia Taarifa Za Usajili NIDA | Hatua kwa hatua

Namna Ya Kuangalia Taarifa Za Usajili NIDA, Kuangalia taarifa...

Mfumo wa Maombi ya Ajira kwa Walimu Mtandaoni (OTEAS)

Mwongozo wa Mfumo wa Maombi ya Ajira kwa Walimu...

Orodha ya Vifurushi vya Azam TV na Bei zake – Chagua Kifurushi Kinachokufaa

Azam TV imekuwa sehemu muhimu ya burudani ndani ya...

Sample/Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Jeshi la Magereza

Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Jeshi la...

Orodha ya Vifurushi vya Azam TV na Bei zake – Chagua Kifurushi Kinachokufaa

Azam TV imekuwa sehemu muhimu ya burudani ndani ya...

Biashara Ndogo Ndogo Zenye Mtaji Kidogo

Biashara Ndogo Ndogo Zenye Mtaji Kidogo, Biashara ndogondogo zenye...

Jinsi ya Kupata Pesa kwa Biashara Ya Upigaji wa Picha Tanzania

Jinsi ya Kupata Pesa kwa Biashara Ya Upigaji wa...

Bei Mpya Vifurushi vya Azam TV | Gharama Mpya za Vifurushi vya Azam TV

Bei Mpya Vifurushi vya Azam TV, Azam TV imekuwa...

Jinsi ya kuandaa Tangazo La biashara kwa urahisi

Jinsi ya kuandaa Tangazo La biashara kwa urahisi, Kuandaa...

Jinsi Ya Kulipia Vifurushi Vya Startimes

Startimes ni moja ya kampuni kubwa za utoaji huduma...

Related Articles

Popular Categories

Njia Rahisi ya Kuangalia Namba ya NIDA Kwa SMS

Njia Rahisi ya Kuangalia Namba ya NIDA Kwa SMS, Kupata namba ya NIDA kwa njia ya SMS ni rahisi na haraka. Njia hii ni...

Jinsi ya Kupata Mtoto wa Kiume

Jinsi ya Kupata Mtoto wa Kiume, Ni shauku ya kila mzazi kupata Watoto wa Jinsia tofauti katika uzao wao ingawaje Wengi hupata watoto wa...

Jinsi ya Kukopa Muda wa Maongezi Halotel | Menu ya kukopa Salio Halotel

Jinsi ya Kukopa Muda wa Maongezi Halotel, Je Unatumia mtandao wa simu wa halotel na umekwama na hujui hatua ,sifa na vigezo za kupata...