Faida za Kusikiliza Muziki Kwenye Maisha

WhatsApp Group Join Now
Telegram Group Join Now

Kusikiliza muziki ni jambo zuri sana maishani na watu wengi Tanzania wanapenda kusikiliza muziki na Tafiti zinabainisha kuwa kusikiliza mziki kuna manufaa mengi kwa ajili ya afya ya mwili na akili.

Faida za Kusikiliza Muziki Kwenye Maisha

Faida za Kusikiliza Muziki Kwenye Maisha

Kusikiliza muziki kuna faida nyingi katika maisha ya kila siku ya binadamu, kiakili, kihisia, kijamii na hata kiafya. Hapa kuna baadhi ya faida kuu za kusikiliza muziki:

1. Mziki Hutufanya Tuwe na Furaha

William James alsisema “Siimbi kwa sababu ninafuraha, bali nafurahi kwa kuwa ninaimba” .

Kusikiliza mziki huzalisha kemikali ya dopamane ambayo hutufanya tujisikie vizuri.

Hii ndiyo sababu mtu akiwa anajisikia vibaya au kukosa furaha mara nyingi anaposikiliza mziki hasa wa taratibu hujisikia vizuri.

SOMA HII  Namna Ya Kuangalia Taarifa Za Usajili NIDA | Hatua kwa hatua

Hivyo basi, wakati ukiwa umekosa raha unaweza kusikiliza nyimbo unazozipenda angalau kwa dakika 15 ili kukuweka katika hali nzuri zaidi.

2. Mziki Huongeza Ufanisi Katika Kukimbia

Mtafiti Marcelo Bigliassi  na wenzake walibaini kuwa wakimbiaji wanaosikiliza mziki walimaliza mbio za mita 800 haraka zaidi kuliko wengine.

Hivyo ni dhahiri kuwa kusikiliza mziki wakati wa kukimbia kunaweza kuwa kama hamasa zaidi.

Unaweza kusikiliza mziki wa haraka haraka au taratibu kulingana na vile unavyopendelea.

3. Mziki Huondoa Msongo na Kuboresha Afya

Kusikiliza mziki hupunguza kwa asilimia 60 homoni zinazosababisha msong stress.

Ikiwa basi msongo utapungua ni dhahiri kuwa pia maradhi mengi ambayo chanzo chake ni msongo yatapungua kama si kwisha kabisa.

Unaweza kusikiliza mziki na kuimba wakati mziki unapoimba; pia usisahau kucheza angalau kwa kuchezesha mguu ili kupata tiba hii kamili.

4. Mziki Hutusaidia Kulala Vizuri

Kusikiliza mziki husafisha ubongo wako na kuuweka katika hali nzuri itakayokuwezesha kupata usingizi mzuri.

SOMA HII  Faida za Kupanga Malengo Kwenye Maisha

Ulishawahi kujiuliza ni kwanini ukisikiliza mziki wa taratibu mara nyingi unapatwa na usingizi? Ni dhahiri kuwa mziki una nafasi kubwa katika kulala kwetu.

Inashauriwa wakati wa usiku kuweka ubongo wako katika hali nzuri ili uweze kulala vyema; unaweza kusikiliza mziki wa taratibu kabla ya kulala.

5. Mziki hukuweka katika hali nzuri unapoendesha gari

Wakati mwingine kuendesha gari ni kazi inayochosha; hivyo inahitaji kiburudisho ili kuifanya vyema.

Ni dhahiri kuwa madereva wanaoendesha magari masafa marefu hupenda kusikiliza mziki ili kujiweka katika hali nzuri.

Hivyo baisi, unaweza kusikiliza mziki unapoendesha gari.

Kumbuka kuzingatia sheria za barabarani; usisikilize kwa sauti kali kiasi cha kushindwa kusikia sauti nyingine barabarani kama vile honi ili kuepuka ajali.

6. Mziki Hutuwezesha Kujifunza

Baadhi ya watu wamebainisha kuwa wanaposoma au kujifunza mambo kadhaa wakati wakisikiliza mziki, basi hufanikiwa kuyamudu maswala hayo vyema.

Si jambo la kustaajabisha kuwaona watu wakisikiliza mziki huku wakisoma vitabu, majarida, tovuti nk.

SOMA HII  Fahamu Gharama za Ushuru wa Kuingiza Gari Kutoka Nje ya Nchi

Hata hivyo, hili linategemea mtu na mtu, wengine hawapendi kusoma au kujifunza huku wakisikiliza mziki, wakati wengine hupenda kufanya hivyo.

Hivyo uamuzi ni wako kuwa unapenda mziki au laa; na ni mziki wa namna gani unaopenda wakati wa kusoma na kujifunza.

7. Mziki Hupunguza Maumivu

Pia utafiti uliofanyika katika chuo cha Drexel cha Philadelphia ulibaini kuwa mziki wa taratibu au wa jadi, hupunguza maumivu kwa wagonjwa wa saratani pamoja na wale walioko katika kitengo cha uangalizi maalumu (ICU).

8. Mziki Hutuhamasisha

Wakati mwingine unakata tamaa au unakutana na mawimbi mengi sana maishani kiasi cha kuzidiwa.

Ni dhahiri ipo miziki inayotia watu moyo na kuwahamasisha.

Ipo mifano ya watu wengi waliotaka kujiua lakini baada ya kusikiliza miziki inayowaeleza umuhimu wa kuendelea mbele na maisha walisitisha mpango wao.

Hivyo kusikiliza mziki kunaweza kukuhamasisha kuendelea kutoka ngazi moja hadi nyingine.

9. Mziki Hutukumbusha Mambo

Ni dhahiri kuwa miziki mingi huambatana na matukio au vipindi fulani vywa muda.

Si jambo la kustajabisha ukasikia mziki fulani ukakukumbusha matukio au eneo fulani ulilokuwa zamani.

Watu wamekuwa wakikumbushwa matukio ya furaha kama vile ndoa, mahafali, au hata ya uzuni kama vile misiba na maradhi.

Hivyo ni wazi kuwa kwa njia ya mziki tunaweza kukumbuka matukio au watu fulani tuliowahi kukutana nao maishani mwetu.

Hot this week

Nafasi za Kazi Jeshi la Magereza 2025

Jeshi la Magereza limetangaza nafasi mpya za ajira kwa...

Namna Ya Kuangalia Taarifa Za Usajili NIDA | Hatua kwa hatua

Namna Ya Kuangalia Taarifa Za Usajili NIDA, Kuangalia taarifa...

Mfumo wa Maombi ya Ajira kwa Walimu Mtandaoni (OTEAS)

Mwongozo wa Mfumo wa Maombi ya Ajira kwa Walimu...

Orodha ya Vifurushi vya Azam TV na Bei zake – Chagua Kifurushi Kinachokufaa

Azam TV imekuwa sehemu muhimu ya burudani ndani ya...

Sample/Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Jeshi la Magereza

Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Jeshi la...

Namna Ya Kuangalia Taarifa Za Usajili NIDA | Hatua kwa hatua

Namna Ya Kuangalia Taarifa Za Usajili NIDA, Kuangalia taarifa...

Jinsi ya Kuhakiki cheti za kuzaliwa eRITA Portal – Hatua Kwa Hatua

Jinsi ya Kuhakiki cheti za kuzaliwa eRITA Portal, Kuhakiki...

Umuhimu/Matumizi ya Kitambulisho cha Taifa NIDA

Matumizi ya Kitambulisho cha Taifa NIDA, Kitambulisho cha Taifa...

Fahamu Gharama za Ushuru wa Kuingiza Gari Kutoka Nje ya Nchi

Fahamu Gharama za Ushuru wa Kuingiza Gari Kutoka Nje...

Umuhimu wa Kupanga Ratiba Kwenye Maisha

Ratiba siyo muhimu tu kwa ajili ya taasisi fulani...

Jinsi ya Kutazama Azam TV Max App Bila Kisimbuzi cha Azam TV

Je, unajua kuwa unaweza kufurahia burudani na huduma za...

Faida za Kupanga Malengo Kwenye Maisha

Faida za Kupanga Malengo Kwenye Maisha, Kujiwekea malengo maishani...

Related Articles

Popular Categories

Njia Rahisi ya Kuangalia Namba ya NIDA Kwa SMS

Njia Rahisi ya Kuangalia Namba ya NIDA Kwa SMS, Kupata namba ya NIDA kwa njia ya SMS ni rahisi na haraka. Njia hii ni...

Jinsi ya Kupata Mtoto wa Kiume

Jinsi ya Kupata Mtoto wa Kiume, Ni shauku ya kila mzazi kupata Watoto wa Jinsia tofauti katika uzao wao ingawaje Wengi hupata watoto wa...

Jinsi ya Kukopa Muda wa Maongezi Halotel | Menu ya kukopa Salio Halotel

Jinsi ya Kukopa Muda wa Maongezi Halotel, Je Unatumia mtandao wa simu wa halotel na umekwama na hujui hatua ,sifa na vigezo za kupata...