Namba ya NIDA inahitajika wakati wa kufungua akaunti za benki, kuomba leseni ya udereva, kupata huduma za matibabu, na hata kushiriki katika masuala ya kijamii kama kupiga kura.
Lengo kuu la mfumo huu ni kuboresha usimamizi wa utambulisho wa raia na kupunguza udanganyifu, hali inayosaidia kuboresha huduma kwa umma kwa ujumla.
Kwa Nini Namba ya NIDA Ni Muhimu Sana Kwa Mtanzania?
Kitambulisho cha NIDA (National Identification Authority) ni hati muhimu sana kwa kila Mtanzania. Kitambulisho hichi ndicho kinatumika kama uthibitisho wa uraia na utambulisho wa mtu. Kitambulisho cha NIDA huitajika kwa mambo mengi, kama vile:
- Huduma za Kibenki: Ili kufungua akaunti au kupata mikopo.
- Ushiriki Katika Uchaguzi: Ili kutekeleza haki ya msingi ya kupiga kura.
- Huduma za Serikali: Ili kupata huduma mbalimbali za serikali.
- Miamala Mingine Muhimu: Kama vile kununua ardhi, kusajili ndoa, na kupata leseni.
- Kusajili Laini za Simu: Namba ya kitambulisho cha NIDA ni lazima wakati wa kusajili laini ya mtandano wa simu yeyote
Hatua za Kuangalia Namba ya NIDA Online kwa haraka
Kuangalia namba ya NIDA mtandaoni ndio njia rahisi, ya haraka, na ya kuaminika zaidi ikilinganishwa na njia zingine kama vile SMS na USSD. Kupitia mtandao, unaweza kupata namba yako bila makato yoyote na kwa uhakika zaidi.
Ili kuangalia namba ya NIDA mtandaoni, unahitaji simu janja au kompyuta yenye uwezo wa kuunganishwa na intaneti.
Njia za Kuangalia Namba ya NIDA Mtandaoni
Hapa kuna njia rahisi za kuangalia namba ya NIDA mtandaoni:
1. Tembelea Tovuti Rasmi: Fungua kivinjari chako cha wavuti na uende kwenye tovuti rasmi ya NIDA: https://services.nida.go.tz/nidportal/get_nin
2. Toa Taarifa Zinazohitajika: Jaza kwa usahihi taarifa zifuatazo:
- Jina la kwanza
- Jina la mwisho
- Tarehe ya kuzaliwa
- Jina la kwanza la mama
- Jina la mwisho la mama
3. Thibitisha Wewe Sio Roboti: Andika neno linaloonyeshwa kwenye picha ili kuthibitisha kuwa wewe si roboti.
4. Pata Namba ya NIDA: Bofya kitufe cha “Angalia” ili kupata namba ya NIDA.