Jinsi ya Kuangalia Salio NSSF Kwa njia ya Simu & Online (NSSF Balance Check)

WhatsApp Group Join Now
Telegram Group Join Now

Wanachama wa NSSF Sasa wanaweza kufuatilia michango yao kujua salio la michango yao Wakiwa nyumbani kwa kutumia simu zao ,Wanaweza kufuatilia Kwa njia ya simu.

Kuhakikisha kuwa unafuatilia salio la akaunti yako ya NSSF (National Social Security Fund) ni muhimu ili kujua jinsi michango yako inavyoendelea na vile vile kujipanga kwa ajili ya mafao yako ya baadaye.

NSSF ni mfuko wa hifadhi ya jamii ambao unatoa huduma muhimu kwa wafanyakazi nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na pensheni, matibabu, na faida nyinginezo. Kuangalia salio lako la NSSF kutakusaidia kujua ni kiasi gani umewekeza kwa ajili ya kustaafu na faida zingine zinazotolewa na mfuko huo.

Neno NSSF limetokana na maneno ya kingereza “National Social Security Fund” ambayo kwa kiswahili ni Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii. NSSF ni taasisi ya serikali ya Tanzania inayohusika na ukusanyaji, uwekezaji, na usambazaji wa michango ya wafanyakazi ili kuhakikisha maisha bora baada ya kustaafu. Ni muhimu kwa kila mfanyakazi kufahamu salio lake ili kupanga mustakabali wake kifedha.

Umuhimu wa Kujua na Kufuatilia Salio la Michango yako NSSF

Kufuatilia salio lako la NSSF ni muhimu kwa sababu:

  • Kujua michango yako: Kuangalia salio la NSSF kutakusaidia kufahamu kama michango yako inafanyika ipasavyo.

  • Kupanga kwa ajili ya kustaafu: Kujua salio lako kutakuwezesha kupanga mipango yako ya baadaye na kufanya maamuzi bora kuhusu fedha zako za kustaafu.

  • Kufuatilia mafao yako: Unaweza kutambua kama unastahili kupata mafao na kuona kama unakubaliana na taarifa za michango yako.

SOMA HII  Jinsi ya Kupata Namba ya NIDA kwa Haraka Zaidi

NSSF Taarifa – Mobile App

Kwa kutumia programu hii utapata taarifa za michango, salio na huduma mbalimbali.

Jinsi ya Kutumia:

• Pakua “NSSF Taarifa” kutoka “Google Play Store”.

• Utapata taarifa binafsi za uanachama.

• Kuangalia taarifa za michango iliyowasilishwa kwenye Shirika bofya “Statements”.

NSSF Taarifa – WhatsApp

Jinsi ya Kutumia:

• Hifadhi namba maalum ya 0756 140 140 kwenye simu.

• Fungua Programu ya WhatsApp kisha tuma ujumbe wa salamu “Hello” au “Habari”.

• Utapokea ujumbe wenye maelekezo ya jinsi ya kutumia huduma hii.

• Andika neno “Statement” kupata taarifa ya michango yote iliyowasilishwa, au tuma neno “Balance” kupata ujumbe wenye salio la michango iliyowasilishwa.

SOMA HII  Jinsi Ya Kuangalia Salio La Vifurushi Airtel

NSSF Taarifa – SMS

Jinsi ya Kutumia:

Ingia ingia kwenye programu ya Ujumbe Mfupi (SMS) kisha tuma ujumbe kwenda namba 15200 kupata huduma zifuatazo:

Kwa Salio/Balance ya michango tuma ujumbe

NSSF SALIO (Namba ya Mwanachama) (Mwaka)

Au

NSSF BALANCE (Member Number) (Year)

Kwa Taarifa/Statement ya michango tuma ujumbe

NSSF TAARIFA (Namba ya Mwanachama) (Mwaka)

Au

NSSF STATEMENT (Member Number) (Year)

Kupitia Huduma za NSSF kwa Wateja (Call Center)

NSSF pia ina huduma ya wateja ambapo unaweza kupiga simu na kuongea na mtumishi wa huduma kwa wateja ili kuangalia salio lako.

  1. Piga simu kwa namba ya huduma kwa wateja: Piga simu kwa namba ya NSSF: 0800 75 00 00.

  2. Zungumza na mtumishi wa huduma kwa wateja: Wafanyakazi wa huduma kwa wateja watakuuliza taarifa za akaunti yako, na kisha watakupa taarifa za salio lako.

SOMA HII  Bei ya Vifurushi Vya Azam kwa Siku

Mfumo wa ‘Member Portal’

Kupitia Mfumo ambao unapatikana katika tovuti ya Shirika yaan www.nssf.go.tz utaweza:

• Kuangalia taarifa za michango yote iliyowasilishwa na Mwajiri wako katika Shirika au michango iliyowasilishwa na mwanachama kwa wanachama wa hiari.

• kupata taarifa za michango (Statements).

Ili upate kuona taarifa zako unatakiwa kuwa namba ya simu ambayo uliisajili NSSF endapo ulibadilisha au haukuiweka tunaomba ufike katika ofisi ya

NSSF iliyojirani yako ili kuweza kuboresha Taarifa zako na kuendelea kufurahia huduma zetu

“NSSF Tunajenga Maisha yako ya Sasa na Baadaye”

Mawasiliano Zaidi na NSSF

Mawasiliano Zaidi na NSSF

Ikiwa unahitaji maelezo zaidi au msaada, unaweza kuwasiliana na huduma kwa wateja wa NSSF kwa kutumia mawasiliano yafuatayo:

  • Barua pepe: customercare@nssf.or.tz
  • Simu: 0 (75) 6140140 | 0800116773 | (255) (22) 2200037
  • Anwani: National Social Security Fund, P.O.Box 1322, Benjamin Mkapa Pension Towers, Azikiwe St, Dar Es Salaam, Tanzania.

 

Hot this week

Nafasi za Kazi Jeshi la Magereza 2025

Jeshi la Magereza limetangaza nafasi mpya za ajira kwa...

Namna Ya Kuangalia Taarifa Za Usajili NIDA | Hatua kwa hatua

Namna Ya Kuangalia Taarifa Za Usajili NIDA, Kuangalia taarifa...

Mfumo wa Maombi ya Ajira kwa Walimu Mtandaoni (OTEAS)

Mwongozo wa Mfumo wa Maombi ya Ajira kwa Walimu...

Orodha ya Vifurushi vya Azam TV na Bei zake – Chagua Kifurushi Kinachokufaa

Azam TV imekuwa sehemu muhimu ya burudani ndani ya...

Sample/Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Jeshi la Magereza

Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Jeshi la...

Namna Ya Kuangalia Taarifa Za Usajili NIDA | Hatua kwa hatua

Namna Ya Kuangalia Taarifa Za Usajili NIDA, Kuangalia taarifa...

Jinsi ya Kuhakiki cheti za kuzaliwa eRITA Portal – Hatua Kwa Hatua

Jinsi ya Kuhakiki cheti za kuzaliwa eRITA Portal, Kuhakiki...

Umuhimu/Matumizi ya Kitambulisho cha Taifa NIDA

Matumizi ya Kitambulisho cha Taifa NIDA, Kitambulisho cha Taifa...

Fahamu Gharama za Ushuru wa Kuingiza Gari Kutoka Nje ya Nchi

Fahamu Gharama za Ushuru wa Kuingiza Gari Kutoka Nje...

Umuhimu wa Kupanga Ratiba Kwenye Maisha

Ratiba siyo muhimu tu kwa ajili ya taasisi fulani...

Jinsi ya Kutazama Azam TV Max App Bila Kisimbuzi cha Azam TV

Je, unajua kuwa unaweza kufurahia burudani na huduma za...

Faida za Kupanga Malengo Kwenye Maisha

Faida za Kupanga Malengo Kwenye Maisha, Kujiwekea malengo maishani...

Related Articles

Popular Categories

Njia Rahisi ya Kuangalia Namba ya NIDA Kwa SMS

Njia Rahisi ya Kuangalia Namba ya NIDA Kwa SMS, Kupata namba ya NIDA kwa njia ya SMS ni rahisi na haraka. Njia hii ni...

Jinsi ya Kupata Mtoto wa Kiume

Jinsi ya Kupata Mtoto wa Kiume, Ni shauku ya kila mzazi kupata Watoto wa Jinsia tofauti katika uzao wao ingawaje Wengi hupata watoto wa...

Jinsi ya Kukopa Muda wa Maongezi Halotel | Menu ya kukopa Salio Halotel

Jinsi ya Kukopa Muda wa Maongezi Halotel, Je Unatumia mtandao wa simu wa halotel na umekwama na hujui hatua ,sifa na vigezo za kupata...