Jinsi Ya Kuchagua Domain Nzuri Ya Biashara, Kuchagua domain nzuri ya biashara (yaani, anwani ya tovuti kama www.jinabishara.com
) ni hatua muhimu sana kwa uwepo wa mtandaoni wa biashara yako.
Domain nzuri husaidia wateja kukupata kwa urahisi, kukuamini, na hata kuathiri nafasi yako kwenye Google (SEO). Domain ni muhimu sana kwa ajili ya utambulisho wa website au blog ya kile unachokifanya.
Inawezekana una majina mengi ambayo unataka uyatumie kama domain ya mtandao ya tovuti au blog yako.
Lakini ni muhimu kufahamu kuwa ukifanya makosa kwenye kuchagua anwani ya mtandao utaathirika kwa kiasi kikubwa.
Madhara ya kukosea kuchagua domain mbaya
- Kutokutambulisha vyema kile unachokifanya
- Kukosa nafasi kwenye injini pekuzi
- Kupoteza wasomaji au watembleaji
- Kuingia kwenye migogoro ya kisheria ikiwa utatumia anzwani inayofanana na za wengine.
Sifa za Domain Bora
1. Domain Lazima iwe na Upekee
Hakikisha unapochagua domain ni ya kipekee sana na inajitambulisha yenyewe.
Usichague anwani ya mtandao kwa sababu kuna nyingine iinayokaribiana nayo, bali chagua ile ambayo itasimama peke yake kwenye domain nyingine.
2. Domain Lazima iwe Ya Kuvutia na kueleweka
Anwani ya mtandao inatakiwa iwe inavutia na kueleweka vyema.
Hakikisha huchagui anwani ya mtandao ambayo ni ngumu kutamkwa, kukumbukwa au kueleweka kwa mtu anayeiona.
Kwa mfano:
- www.pesazakoltdtz.com – Ni anwani ya mtandao mbaya
- www.habari24hrsleo.com – Ni anwani ya mtandao mbaya
Badala yake zingeweza kuwa:
- www.pesazako.com, www.pesazakoltd.com, www.habari24hrs.com au www.habari24.com
Naamini umeona mifano hiyo hapo juu ilivyokiuka swala la kuvutia na kueleweka vyema.
3. Usitumie Namba au Alama Ambazo Sio Herufi
Anwani ya mtandao nzuri haitakiwi kuwa na namba au alama ambazo siyo herufi kwani itawachanganya watumiaji pamoja na kutokupata nafasi vyema kwenye injini pekuzi.
Mifano ya domain ambazo zimetumia namba na alama nyingine.
www.chakula2953.com, www.nguo-za_watoto-na-vijana.com.
Ni wazi kuwa anwani kama hizi ni vigumu kukuwezesha kufikia lengo lako kupitia tovuti au blog yako.
4. Lazima Ufikirie Matumizi Ya Mbeleni
Usinunue anwani ya mtandao amabayo haitoweza kukufaa miaka kadhaa ijayo.
Epuka kuweka vitu vinavyopita, matukio au watu kwenye anwani ya tovuti au blog yako, kwani vikipita na anwani yako itakuwa imekosa thamani.
Kwa mfano: www.kanumbashop.com, www.prisonbreakmobiles.com, n.k ni baadhi anwani mbaya.
5. Usitumie Jina Lako Kama Sio Lazima
Watu wengi hupenda kutumia majina yao kama vile www.johjuma.com, www.rosemoshe.net, n.k. kwenye anwani za tovuti au blog zao, lakini jambo hili siyo zuri sana.
Je jina lako ndilo jina la kampuni au kile unachokifanya? Je watu wanaotafuta vitu kwenye injini pekuzi kama google watatafuta jina lako ili liwawezeshe kufikia tovuti yako, je ni blog binafsi?
Ikiwa majibu ya maswali yaliyoulizwa hapa ni hapana, basi hakuna haja ya kutumia jina lako kwenye anwani ya tovuti au blog yako.
6. Domain Lazima itambulishe Kile Unachokifanya
Kama nilivyoeleza kwenye hoja zilizopita, hakikisha unachagua anwani ambayo inatambulisha vyema kile unachokifanya.
Kumbuka tovuti au blog iliyotengenezwa vyema inaweza kuwa chanzo chako cha kile unachokifanya kufahamika vyema na hatimaye kuongeza mauzo na faida.
Kwa mfano kama unafanya biashara ya chakula unaweza kuwa na anwani kama vile: www.chakulabora.com, www.msosimurwa.com, www.onjamapishi.com, n.k
7. Usiige za Domain za Watu Wengine
Kuna watu wanafikiri kuiga anwani za tovuti au blog kubwa ndiko kufanikiwa lakini mambo yamekuwa ndivyo sivyo.
Unapoiga anwani ya tovuti nyingine unaonyesha kuwa huna uwezo mzuri wa ubunifu na pili unaweza kuingia kwenye migogoro ya kisheria kati yako na wale uliowaiga.
Kwa mfano ukisajili anwani inayoitwa www.facebook.co.tz au co.ke utaingia kwenye mgogoro na Facebook hata kama umeilipia pesa.
8. Jitahidi Kuchagua Domain Fupi
Anwani ndefu ni vigumu kukumbukwa au kuandikwa kwa usahihi. Hivyo ni muhimu kuzingatia kuchagua anwani fupi na nzuri inayoeleweka.
Epuka anwani kama vile www.nunuagarizurikwaajiliyako.com au www.patahabarimotomotokilawakati.com.
9. Domain Lazima iwe na Gharama Ndogo
Mara nyingi anwani za mtandao huanzia gharama ya dola 5 hadi 500+. Hivyo ni muhimu kuhakikisha unachagua anwani ya mtandao ambayo unamudu gharama zake.
10. Domain Lazima iwe na Extension Nzuri
Kila anwani ya mtandao ina kikamilisho chake kama vile .com, .net, .org, .info, n.k. na kila kimoja kina maana yake kulingana na mahitaji ya mwenye tovuti au blog.
Ikumbukwe pia vikamilisho vya anwani ya mtandao ndivyo huamua bei ya anwani husika.
Hakikisha unachagua kikamilisho ambacho kinaendana na kile unachokifanya ili anwani yako ikuelezee vyema.
MBINU ZA KUCHAGUA DOMAIN NZURI
1. Tumia Jina la Biashara Moja kwa Moja
-
Mfano:
ZuriFashions.co.tz
,SmartTechTz.com
2. Tumia Keyword ya Biashara
-
Kama jina lako halipatikani, tumia neno linaloelezea huduma zako.
-
Mfano:
nywelezaaisha.com
,safitouchtz.co.tz
3. Angalia Upatikanaji Mtandaoni
- Tumia tovuti kama:
- godaddy.com
- namecheap.com
- hostafrica.co.tz – kwa
.co.tz
4. Weka Akiba ya Majina Mengine Kama Yapo
-
Kama unaweza, nunua
.com
na.co.tz
kwa jina moja ili mtu mwingine asilitumie.
MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUNUNUA DOMAIN
- Fanya utafiti: Je, jina hilo limeshatumika na mtu mwingine?
- Lilinganishe na jina lako la biashara lililosajiliwa BRELA (ikiwa lipo).
- Kagua kama jina hilo halihusiani na biashara haramu au linaloweza kuleta utata.
Mfano wa Domain Nzuri kulingana na Biashara:
Aina ya Biashara | Domain Nzuri |
---|---|
Saluni ya Urembo | glamtouch.co.tz / glamtouch.com |
Huduma za Usafi | saficlean.co.tz |
Mgahawa | tamubites.com / tamubites.co.tz |
Mavazi ya Mitumba | urbanmitumba.co.tz |
Uuzaji wa Simu | mobitech.co.tz / buysimu.com |