Jinsi ya Kukopa Muda wa Maongezi Halotel, Je Unatumia mtandao wa simu wa halotel na umekwama na hujui hatua ,sifa na vigezo za kupata mkopo na salio kutoka Halotel? usijali makala hii itaupitisha kufaham kila kitu kuhusiana na Kukopa salio halotel.
Ili kukopa muda wa maongezi Halotel, fuata hatua rahisi zifuatazo. Huduma hii inaitwa “Halotel Halo Advance” – inakuwezesha kupata mkopo wa muda wa maongezi au data pale unapokuwa huna salio la kutosha.
Kupitia menu ya kukopa salio Haloteli ni *149*63# mteja wa halotel anaweza kukopa salio mda wowote anapohitaji.
Vigezo vya Kukopa Halotel
- Lazima uwe mteja wa Halotel kwa angalau siku 90 (miezi 3).
- Uwe unatumia huduma za Halotel mara kwa mara.
- Uwe hauna mkopo wa awali ambao bado hujalipa.
- Sim yako iwe imesajiliwa kikamilifu.
Jinsi ya Kukopa Muda wa Maongezi halotel
1. Piga *149*63# kwenye Simu Yako
Kuanza mchakato wa kukopa muda wa maongezi Halotel, piga 14800# kwenye simu yako ya Halotel. Hii itaanzisha menyu maalum ya kukopa muda wa maongezi.
2. Chagua Chaguo la “Kukopa Salio”
Baada ya kuingia menyu, chagua chaguo la “Kukopa Muda wa Maongezi” kutoka kwenye orodha ya huduma zinazopatikana. Hii itakuleta kwenye hatua inayofuata ya mchakato.
3. Chagua Kiwango cha Muda wa Maongezi Unachotaka
Kwenye hatua hii, utapewa chaguo la kuchagua kiwango cha muda wa maongezi unachotaka kukopa. Chagua kiwango kinachokidhi mahitaji yako na bonyeza OK au Tuma ili kuhakikisha kukopa muda wa maongezi.
4. Thibitisha Ombi Lako
Baada ya kuchagua kiwango cha muda wa maongezi, utaombwa kuthibitisha ombi lako. Hakikisha unaangalia vizuri maelezo yaliyoonyeshwa kwenye skrini na kuthibitisha ombi lako.
Huduma kwa Wateja Halotel
Ikiwa unapata shida kukopa au hauna uhakika na salio/deni lako:
- Piga: 100
- Au tembelea duka la Halotel lililo karibu nawe.