Jinsi ya Kununua Tiketi za Mpira kwa Kutumia Airtel Money, Airtel Money ni huduma ya kifedha inayotolewa na kampuni ya Airtel, ambayo inawawezesha wateja wake kufanya malipo, kutuma fedha, na kupokea pesa kwa kutumia simu zao za mkononi.
Huduma hii inafanya ununuzi wa tiketi za mpira kuwa rahisi, haraka, na salama bila ya haja ya kwenda kwenye maduka ya tiketi au kusubiri katika foleni ndefu.
Jinsi ya Kununua Tiketi za Mpira Airtel Money
Zifuatazo ni hatua za Kununua Tiketi za Mpira kwa Airtel Money
Piga *150*60#
Anza kwa kupiga *150*60# kwenye simu yako. Hii itakupeleka moja kwa moja kwenye menyu ya Airtel Money.
Chagua 5 > Lipa Bill
Baada ya kuingia kwenye menyu ya Airtel Money, chagua namba 5 ambayo ni “Lipa Bill”.
Chagua # > Next
Chagua # ili kuendelea na hatua inayofuata.
Chagua 8 > Malipo Mtandao
Kwenye menyu inayofuata, chagua namba 8 ambayo ni “Malipo Mtandao”.
Chagua 1 > Tiketi za Michezo
Chagua namba 1 kwenye menyu ya “Tiketi za Michezo”.
Chagua 1 > Football Tickets
Baada ya hapo, chagua namba 1 kwa “Football Tickets”.
Chagua Mechi Unayotaka Kulipia
Kwenye orodha ya mechi zinazopatikana, chagua mechi unayotaka kulipia tiketi.
Chagua Aina ya Tiketi Unayotaka Kulipia
Baada ya kuchagua mechi, utaulizwa uchague aina ya tiketi unayotaka kulipia.
Weka Namba ya Kadi yako ya (N-Card)
Weka namba ya kadi yako ya N-Card ili kukamilisha mchakato wa malipo.
Ingiza Namba ya Siri
Ingiza namba yako ya siri ya Airtel Money ili kuthibitisha malipo.
Thibitisha
Hatua ya mwisho ni kuthibitisha malipo yako. Utapokea ujumbe wa kuthibitisha kuwa malipo yako yamekamilika na tiketi yako imekatwa.