Mambo ya kuzingatia katika Kuchagua Eneo Zuri La Biashara

WhatsApp Group Join Now
Telegram Group Join Now

Kuchagua eneo zuri la biashara ni moja ya mambo muhimu sana yanayoathiri mafanikio au kushindwa kwa biashara. Eneo sahihi huongeza wateja, hufanikisha upatikanaji wa bidhaa/huduma kwa urahisi, na hupunguza gharama zisizo za lazima.

Hapa chini ni mambo muhimu ya kuzingatia unapochagua eneo la kuanzisha biashara.

Mambo ya kuzingatia katika Kuchagua Eneo Zuri La Biashara

Mambo ya kuzingatia katika Kuchagua Eneo Zuri La Biashara

Jinsi ya kuchagua sehemu ya biashara kwa Tanzania ni muhimu sana kwasababu itachangia na kuongeza mafanikio ya kwenye biashara.

1. Angalia Ushindani wa Biashara

Ushindani ni jambo muhimu sana linaloweza kufanya eneo la biashara kuwa zuri au baya. Hebu fikiri mtu mchanga kabisa anaanzisha biashara mahali ambapo tayari kuna wafanyabiashara wengine wakubwa wenye uzoefu, mtaji, vitendeakazi au hata mtandao mzuri wa washirika.

SOMA HII  Orodha ya Taasisi za Mikopo Mkoa wa Dar es salaam

Bila shaka, itakuwa vigumu sana kwa mtu huyo kukua kibiashara. Ni lazima mtu apime na achague eneo amabalo lina ushindani ambao anaweza kuumudu na kukua.

2. Uhusiano kati ya biashara na mazingira

Mara nyingi biashara huhusiana na mazingira husika. Kwa mfano ni rahisi kufanikiwa kwenye biashara ya stationary kwenye maeneo ya vyuo, shule au taasisi kuliko nje ya mazingira hayo.

Kwa mfano pia ni rahisi mtu kuendesha biashara ya vyinywaji na vitafunwa, vipodozi na simu kwenye kituo cha mabasi kuliko biashara ya nafaka au pembejeo.

Hivyo ni muhimu kupima kama biashara yako itaendana na eneo husika unalotaka kulichagua.

3. Mtindo wa maisha katika eneo husika

Kila eneo lina mtindo wake wa maisha. Itakuwa jambo la kusikitisha sana wewe kufungua biashara ambayo bidhaa yake ndogo kabisa ni shilingi 100,000 na wakati nguvu ya ununuzi ya watu wa eneo husika ni 1,000.

Ngoja nikupe mfano rahisi zaidi, kwa mfano watu waliozoea kununua mafuta ya mia tano, unga robo na sabuni kipande, ukifungua supermarket katika eneo hilo ni wazi kuwa utakosa wateja hatakama unauza bidhaa nzuri kiasi gani.

SOMA HII  Jinsi Ya Kutoa Huduma Nzuri Kwa Mteja Kwenye Biashara

4. Wingi wa waakazi

Wingi wa watu katika eneo husika ni sawa sawa na mauzo zaidi au kuonekana zaidi kwa biashara yako. Haijalishi eneo lina fremu nzuri au za gharama nafuu kiasi gani, kama halina wakaazi wa kutosha litakuchelewesha sana kufikia malengo yako.

Ikiwa ni eneo ambalo watu wanahamia kwa kasi kubwa kwa kipimo kuwa ndani ya muda mfupi utakuwa na wateja wengi basi hapo unaweza kuvumilia; lakini kama eneo ndivyo lilivyo nyumba moja ipo baada ya mita 500 basi hilo halikufai.

5. Miundo mbinu na huduma za kijamii

Unapoangalia eneo la kufanyia biashara ni zaidi ya kile chumba au nyumba unayoichagua kuitumia kama ofisi yako.

Itakuwa si jambo la busara kuendesha biashara inayohitaji maji au umeme wa kutosha mahali ambapo hakuna huduma hizo.

Pima hili mapema lisije likakusababishia changamoto au gharama kubwa za uendeshaji zisizokuwa na ulazima.

Hakikisha pia eneo hilo linafikika katika vipindi vyote vya mwaka. Kwa mfano itakuwa nijambo la ajabu mtu kufungua biashara ya kuuza gesi kwenye eneo ambalo liko uchochoroni; kiasi kwamba hata yale magari ya gesi hayawezi kufika au hata wateja wake wanamfikia kwa taabu.

Hivyo, fanya tathimini ya miundombinu kwa kina.

6. Usalama na majirani

Usalama ni nguzo muhimu sana katika kujenga mazingira mazuri ya kibiashara.  Hakuna mteja atakayependa kuja kwenye biashara ambayo atajihisi kutokuwa salama.

SOMA HII  Orodha ya Vifurushi vya Azam TV na Bei zake - Chagua Kifurushi Kinachokufaa

Mfanyabiasha naye hawezi kufanikiwa ikiwa anafanya biashara kwenye mazingira ambayo siyo salama kwake na mali zake.

Hakikisha pia mazingira yanayokuzunguka, majirani pamoja na biashara za jirani hazitaathiri biashara yako. Kwa mfano siyo biashara zote zinaweza kufanywa karibu na biashara kama vile baa, karakana ya ufundi n.k.

Nimeshuhudia watu wakiacha fremu zao za biashara kutokana na kuzungukwa na majirani wabaya; nimeshuhudia watu wakigomeana kulipa luku, maji n.k. hadi kufikia kuziacha biashara zao.

Hivyo tafakari sana kabla ya kuchagua eneo la biashara.

7. Gharama za uendeshaji wa eneo husika

Haijalishi eneo la biashara ni zuri au umelipenda kwa kiasi gani, ni lazima ulinganishe kama gharama za uendeshaji zinazotokana na kufanya biashra kwenye eneo husika zitalipa.

Inawezekana umekutana na mwenye nyumba anayepangisha fremu yake nzuri sana kwa shilingi 500,000 kwa mwezi, kumbe ni ili alipe mkopo wake wa bank; lakini katika uhalisia biashra katika eneo hilo haiwezi kufikisha mauzo ya 50,000 kwa siku.

Ukidanganyika kwa  mazingira hapa bila kupima uhusiano wake na gharama za uendeshaji utakuwa na wakati mgumu sana.

8. Mahitaji ya kipekee ya biashara husika

Suala hili hupuuziwa sana na watu wengi wanapotaka kuanzisha biashara, lakini huwaletea changamoto kubwa. Ni muhimu sana ufahamu biashara yako ina mahitaji gani ya kipekee ya sasa na baadae.

Hot this week

Nafasi za Kazi Jeshi la Magereza 2025

Jeshi la Magereza limetangaza nafasi mpya za ajira kwa...

Namna Ya Kuangalia Taarifa Za Usajili NIDA | Hatua kwa hatua

Namna Ya Kuangalia Taarifa Za Usajili NIDA, Kuangalia taarifa...

Mfumo wa Maombi ya Ajira kwa Walimu Mtandaoni (OTEAS)

Mwongozo wa Mfumo wa Maombi ya Ajira kwa Walimu...

Orodha ya Vifurushi vya Azam TV na Bei zake – Chagua Kifurushi Kinachokufaa

Azam TV imekuwa sehemu muhimu ya burudani ndani ya...

Sample/Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Jeshi la Magereza

Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Jeshi la...

Orodha ya Vifurushi vya Azam TV na Bei zake – Chagua Kifurushi Kinachokufaa

Azam TV imekuwa sehemu muhimu ya burudani ndani ya...

Biashara Ndogo Ndogo Zenye Mtaji Kidogo

Biashara Ndogo Ndogo Zenye Mtaji Kidogo, Biashara ndogondogo zenye...

Jinsi ya Kupata Pesa kwa Biashara Ya Upigaji wa Picha Tanzania

Jinsi ya Kupata Pesa kwa Biashara Ya Upigaji wa...

Bei Mpya Vifurushi vya Azam TV | Gharama Mpya za Vifurushi vya Azam TV

Bei Mpya Vifurushi vya Azam TV, Azam TV imekuwa...

Jinsi ya kuandaa Tangazo La biashara kwa urahisi

Jinsi ya kuandaa Tangazo La biashara kwa urahisi, Kuandaa...

Jinsi Ya Kulipia Vifurushi Vya Startimes

Startimes ni moja ya kampuni kubwa za utoaji huduma...

Related Articles

Popular Categories

Njia Rahisi ya Kuangalia Namba ya NIDA Kwa SMS

Njia Rahisi ya Kuangalia Namba ya NIDA Kwa SMS, Kupata namba ya NIDA kwa njia ya SMS ni rahisi na haraka. Njia hii ni...

Jinsi ya Kupata Mtoto wa Kiume

Jinsi ya Kupata Mtoto wa Kiume, Ni shauku ya kila mzazi kupata Watoto wa Jinsia tofauti katika uzao wao ingawaje Wengi hupata watoto wa...

Jinsi ya Kukopa Muda wa Maongezi Halotel | Menu ya kukopa Salio Halotel

Jinsi ya Kukopa Muda wa Maongezi Halotel, Je Unatumia mtandao wa simu wa halotel na umekwama na hujui hatua ,sifa na vigezo za kupata...