Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, leo kitashuka dimbani kupambania nafasi ya kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya CHAN 2024 ambapo kitachuana na mabingwa wa soka barani Afrika, Morocco, katika mtanange wa kukata shoka unaotarajiwa kutimua vumbi katika dimba la Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam majira ya saa 2:00 usiku.
Mashabiki wa soka kote nchini wanasubiri kwa hamu matokeo ya Taifa Stars vs Morocco leo 22/08/2025 CHAN ili kuona kama Stars wataandika historia mpya ya kufika nusu fainali kwa mara ya kwanza.
Matokeo ya Taifa Stars vs Morocco Leo 22/08/2025 CHAN
Tanzania | VS | Morocco |
Friday, August 22, 2025
👕 | Tanzania 🇹🇿 ✖ 🇲🇦 Morocco
🏆 | CHAN 2024 – Quarter-finals
⏰ | 20:00 🇹🇿
🏟️ | Benjamin Mkapa Stadium – Dar Es Salaam
Safari ya Taifa Stars na Morocco Kufika Robo Fainali
Tanzania ilimaliza kileleni mwa Kundi A ikiwa na pointi 10 baada ya kushinda mechi tatu na kutoka sare moja, rekodi ambayo imewapa nafasi ya kipekee kwenye robo fainali.
Kwa upande wa Morocco, walimaliza nafasi ya pili Kundi A wakiwa na pointi 9, wakishinda mechi tatu na kupoteza moja dhidi ya Kenya. Waliwafunga Angola 2-0, wakaangukia kwa Kenya 0-1, kisha kuibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Historia ya Taifa Stars dhidi ya Morocco
Mchezo wa leo utakuwa ni mara ya nane kwa Taifa Stars na Morocco kukutana kwenye mashindano rasmi. Morocco wana rekodi nzuri zaidi wakiwa wameshinda michezo sita, huku Tanzania ikishinda mchezo mmoja pekee na hakuna sare kati ya timu hizo.