Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi ya Mtendaji wa Kijiji, Fahamu Jinsi ya kuandika Barua ya kuomba kazi za Afisa utendaji kata,tarafa ,utendaji vijiji na Halmashauri makala hii imeorodhesha vitu muhimu katika kuandika barua pamoja na mfano wa barua tumekuwekea ili kujifunza jinsi barua inavyotakiwa kuwa kimpangilio na muonekano.
Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imekua ikitangaza nafasi za kazi za mtendaji wa kijiji na mitaa kwa wilaya mbalimbali Tanzania. Kama wewe umekidhi vigezo vya kua mtendaji wa mtaa au kijiji, nafasi hizi za kazi ni fursa nzuri ya kukuwezesha kutumikia wananchi huku ukijipatia mshahara wa kukidhi mahitaji ya kila siku.
Nafasi nyingi za kazi za Mtendaji wa kijiji katika halmashauri za wilaya mbalimbali Tanzania maranyingi huitaji mwombaji mwenye elimu ya kidato cha nne (form iv) au sita(form six) aliyehitimu astashahada/cheti katika moja ya fani zifuatazo:
Utawala, sheria, Elimu ya jamii,usimamizi wa fedha, maendeleo ya jamii na sayansi ya sanaa kutoka chuo cha serikali za mitaa hombolo au chuo chochote kinachotambuliwa na serikali.
Kama umekidhi sifa hizo, basi ni vyema kuanza mchakato wa kutuma maombi. Mchakatoi wa kutuma maombi ya kazi kwa nafasi za mtendaji wa kijiji maranyingi huanza na zoezo la kuandika barua ya maombi ya kazi. Kwa kutambua umuhimu wa kuandika barua ya kazi kwa usahihi, hapa Habariforum tumekuletea mifano ya barua za kazi TAMISEMI kwa nafasi za ajira za mtendaji wa kijiji na mtaa.
Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mtendaji wa Kijiji na Mtaa
Muundo wa Barua ya Maombi ya Kazi
- Anuani ya mwandishi. Yaani anuani yako wewe unayeandika barua hiyo.
- Tarehe.
- Anuani ya anayeandikiwa.
- Salamu.
- Kichwa cha habari.
- Kiini cha barua. Hii ni roho ya barua yako, ukikosea mahali hapa, kama unajibu swali katika mtihani, utapoteza alama. Na kama unaomba kazi halisi, utaikosa. Kiini kina aya nne:
- – Katika aya ya kwanza, eleza kazi unayoomba na mahali ulipoona tangazo la kazi hiyo. Ni katika sehemu hii unaweza kutaja umri wako.
- – Katika aya ya pili, eleza ujuzi wako kwa ufupi. Usieleze sana. Barua hii haipaswi kuwa ndefu kupindukia.
- – Aya ya tatu eleza kwa nini upewe kazi hii wewe na si mtu mwingine. Epuka kueleza shida zako binafsi ili upewe kazi. Maneno kama, ninaomba kazi hii ili niweze kumtibia mama yangu mgonjwa kitandani,hayana msaada.
- – Aya ya nne eleza uko tayari kwa usahili siku gani?
- Mwisho wa barua. Mwisho wa barua yako uwe na:
- – Neno la kufungia. Wako mtiifu. Wako katika ujenzi wa taifak
- – Sahihi yako.
- – Jina lako
Wengine hujifunza kuandika barua ya maombi ya kazi ili waweze kujibu maswali katika mtihani, na wengine hujifunza ili waweze kuandika barua hizo, waweze kuomba kazi halisi. Vyovyote vile, mfano huu halisi wa barua, ni sahihi kwa watu wote, wanafunzi na wale wanaotafuta kazi.