Je, umewahi kukumbana na aibu ya kuombwa namba yako ya simu lakini ukashindwa kuikumbuka? Usijali, sio wewe pekee ambae umeshawahi tokewa na hii hali! Kutokana na umuhimu wa kujua namba ya simu tunayotumia, tumekuandalia mwongozo rahisi wa jinsi ya kuangalia namba yako ya simu kwa haraka, bila kujali mtandao unaotumia
Muongozo huu unaangazia
- Jinsi ya kujua namba ya simu ttcl
- Jinsi ya kujua namba ya simu YAS
- Jinsi ya kujua namba ya simu halotel
- Jinsi ya kujua namba ya simu airtel
Namna Ya Kuangalia Namba Ya Simu Airtel, Vodacom, TTCL, YAS & Halotel
Kuna njia kadhaa za kuangalia namba yako ya simu kutegemeana na mtandao unaotumia (kama ni Safaricom, Airtel, YAS, Halotel, Vodacom, n.k.). Hapa chini nimeweka njia za kawaida kwa mitandao maarufu:
Kwa Kutumia USSD Code
Hii ndiyo njia rahisi zaidi ya kuangalia namba yako:
- Vodacom (Tanzania)
- Piga:
*106#
- Chagua: “Taarifa Binafsi”
- Kisha chagua “Angalia namba yangu”
- Piga:
- YAS (Tanzania)
- Piga:
*102*2#
- Au
*255*4*1#
- Piga:
- Airtel (Tanzania)
- Piga:
*106#
- Chagua: “Taarifa binafsi” → “Namba yangu”
- Piga:
- Halotel (Tanzania)
- Piga:
*150*88#
- Chagua: “Taarifa Binafsi”
- Piga:
- Zantel
- Piga:
*#62#
au*100#
kisha fuata maelekezo.
- Piga:
Kupiga Simu au Kutuma SMS kwa Rafiki
-
Mpigie mtu unayemjua au mtumie SMS, aone namba yako na akuambie.
Kupitia Sim Settings (kwa simu za Android/iPhone)
-
Android:
- Nenda kwenye Settings > About phone > SIM status
- Mara nyingi utaona namba ya simu hapo (lakini si mara zote huonekana)
-
iPhone:
-
Nenda Settings > Phone > My Number
-
Angalia kwenye laini/simu box
-
Wakati mwingine namba ya simu huwa imeandikwa kwenye kadi ya laini (SIM card holder) uliyopatiwa uliponunua laini.
Nchini Tanzania, watoa huduma wote wa mtandao hutumia namba sawa, kwa hivyo hatua zilizo hapa chini zitatumika kwa watoa huduma wote wa simu:
- Ili kuangalia namba ya simu Piga *106#
- Chagua #1 “Angalia Usajili”
- Kisha utaona nambari yako ya simu pamoja na jina kamili lililotumika kusajili SIM Kadi