Nauli ya Basi Dar Es Salaam kwenda Morogoro, Miongoni mwa makampuni maarufu yanayo toa huduma ya kusafirisha abiria kutoka dar es salaam kwenda Morogoro ni BM, Abbood Bus, New force, shabibi line, Kimbinyiko n.k. Makampuni haya yamekua yakitoza nauli kulingana na viwango vilivyopangwa na LATRA (Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini).
Kama wewe ni miongoni mwa maelfu ya wasafiri wanaotarajia kusafiri kutoka jiji la kibiashara Dar es Salaam hadi kitovu cha kilimo Morogoro, na ungependa kujua nauli za mabasi, basi umefika mahali sahihi. Tumekusanya taarifa kamili kuhusu nauli za mabasi kama zilivyopangwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA).
Nauli ya Basi Dar Es Salaam kwenda Morogoro
Hadi hii leo May , nauli za mabasi kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro zimewekwa kama ifuatavyo kulingana na aina ya basi na mamlaka husika (LATRA):
Aina ya Basi | Nauli (Tsh) | Umbali (km) |
Basi la kawaida (Ordinary) | 9,000 | 192 |
Basi la kifahari (Luxury) | 13,000 | 192 |
Tafadhali kumbuka kwamba nauli hizi zinaweza kubadilika kidogo kulingana na kampuni ya basi unayochagua kusafiri nayo. Baadhi ya kampuni huenda zikatoza kiasi kidogo zaidi au kidogo chini ya bei hizi elekezi za kawaida.
Ili kupata taarifa ya uhakika zaidi kuhusu nauli za mabasi, tunashauri uwasiliane moja kwa moja na kampuni ya basi unayotaka kusafiri nayo au kutembelea tovuti yao rasmi. Unaweza kununua tiketi yako moja kwa moja kwenye vituo vya mabasi au kupitia tovuti za kampuni za mabasi husika. Inashauriwa kununua tiketi mapema, hasa wakati wa misimu ya kusafiri yenye wasafiri wengi, ili kuepuka usumbufu wowote.