Orodha ya Wafungaji Bora CHAN 2025, Michuano ya CHAN 2025 imefikia hatua ya robo fainali ambapo mataifa nane yameibuka videdea baada ya kujikatia tiketi ya kuendelea kupambana katika hatua ya mtoano.
Sambamba na mvuto wa mechi hizi, mbio za Wafungaji Bora CHAN 2025 | Vinara wa Magoli CHAN 2024/2025 zimeendelea kushika kasi, huku washambuliaji kadhaa wakionyesha makali yao katika hatua ya makundi.
Mashindano haya ya ubingwa wa mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani yanashirikisha jumla ya mataifa matatu wenyeji Uganda, Tanzania na Kenya na yanatarajiwa kufikia tamati ifikapo Agosti 30, 2025.
Timu Zilizofuzu Robo Fainali CHAN 2025
Baada ya hatua ya makundi kukamilika, timu nane zimefanikiwa kutinga robo fainali kwa ushindani mkali. Kila kundi lilitoa timu mbili bora ambazo sasa zitapambana ili kufuzu nusu fainali. Mechi za robo fainali zitakazochezwa ni kama ifuatavyo:
- Kenya × Madagascar
- Tanzania × Morocco
- Uganda × Senegal
- Sudan × Algeria
Matarajio ni makubwa huku kila taifa likilenga si tu kutwaa ubingwa, bali pia kutoa mfungaji bora wa mashindano haya.
Wafungaji Bora CHAN 2025 | Vinara wa Magoli CHAN 2024/2025
Mbio za Wafungaji Bora CHAN 2025 zimekuwa na ushindani mkubwa. Baada ya hatua ya makundi, wachezaji watatu wanaongoza kwa mabao matatu kila mmoja, wakifuatiwa na kundi la wachezaji kadhaa wenye mabao mawili.
Wachezaji wanaoongoza kwa mabao 3
- Thabiso Kutumela (Afrika Kusini) – Mabao 3
- Allan Okello (Uganda) – Mabao 3
- Oussama Lamlioui (Morocco) – Mabao 3
Wachezaji waliopachika mabao 2
- Lalaina Cliver Rafanomezantsoa (Madagascar) – Mabao 2
- Mohamed Rabii Hrimat (Morocco) – Mabao 2
- Jephté Kitambala (DR Congo) – Mabao 2
- Sofiane Bayazid (Algeria) – Mabao 2
- Kaporal (Angola) – Mabao 2
- Clément Mzir (Tanzania) – Mabao 2
- Austin Odhiambo (Kenya) – Mabao 2
- Ryan Ougam (Kenya) – Mabao 2
- Abdelrahman Omar (Sudan) – Mabao 2