Putin Agoma Kukutanishwa na Zelensicky Ikulu ya Urusi

WhatsApp Group Join Now
Telegram Group Join Now

Putin Agoma Kukutanishwa na Zelensicky Ikulu ya Urusi

Putin agoma kukutanishwa na Zelensicky Ikulu ya Urusi imepuuzilia mbali mazungumzo ya kufanyika kwa mkutano kati ya Rais wa Urusi, Vladimir Putin, na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, licha ya wito uliotolewa na Rais wa Marekani, Donald Trump, akihimiza viongozi hao kukutana ili kujadili kumaliza vita nchini Ukraine.

Shinikizo la kufanyika kwa mazungumzo hayo linakuja baada ya Trump kukutana na Putin mjini Alaska wiki iliyopita, na kisha kuwakaribisha viongozi saba wa Ulaya pamoja na Zelensky katika Ikulu ya White House siku ya Jumatatu.

Trump alikiri mzozo huo ni “vigumu” kusuluhisha, huku akionya kuwa huenda Rais Putin hakutaka kumaliza uhasama. “Tutajua kuhusu Rais Putin katika wiki kadhaa zijazo. Inawezekana kwamba hataki kufanya makubaliano,” alisema Jumanne. Aidha, aliongeza kuwa Putin anapitia “wakati mgumu” bila kutoa maelezo zaidi.

SOMA HII  Ramani ya Jengo Jipya la Makao Makuu ya CCM Lenye Thamani ya TSh 34 Bilioni

Siku ya Jumatatu, Putin alimwambia Trump kuwa yuko “sawa” na wazo la mazungumzo ya moja kwa moja na Ukraine, lakini siku iliyofuata Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov, alilitupilia mbali pendekezo hilo, akisisitiza kuwa mkutano wowote lazima utayarishwe hatua kwa hatua kuanzia ngazi ya wataalam.

Dmitry Polyanskiy, Naibu Mwakilishi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa, alikiambia chombo cha habari cha BBC kuwa “hakuna mtu aliyekataa” uwezekano wa mazungumzo ya moja kwa moja, lakini akaonya kuwa “haipaswi kuwa mkutano kwa ajili tu ya mkutano uwe umefanyika.”

Wakati huo huo, taarifa zilidai kwamba Putin alipendekeza kwa Trump kuwa Zelensky asafiri hadi Moscow kwa mazungumzo, pendekezo ambalo Ukraine ilikataa mara moja. Wachambuzi wanasema hatua hiyo inaweza kuwa mbinu ya Urusi kuweka sharti lisilowezekana ambalo Ukraine haiwezi kulikubali.

SOMA HII  Vyama 17 Vyachukua Fomu Urais wa Zanzibar, CHADEMA & CHAUMMA hawajajitokeza

Hot this week

Nafasi za Kazi Jeshi la Magereza 2025

Jeshi la Magereza limetangaza nafasi mpya za ajira kwa...

Namna Ya Kuangalia Taarifa Za Usajili NIDA | Hatua kwa hatua

Namna Ya Kuangalia Taarifa Za Usajili NIDA, Kuangalia taarifa...

Mfumo wa Maombi ya Ajira kwa Walimu Mtandaoni (OTEAS)

Mwongozo wa Mfumo wa Maombi ya Ajira kwa Walimu...

Orodha ya Vifurushi vya Azam TV na Bei zake – Chagua Kifurushi Kinachokufaa

Azam TV imekuwa sehemu muhimu ya burudani ndani ya...

Sample/Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Jeshi la Magereza

Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Jeshi la...

Mahakama Yazuia Kurushwa Mubashara Ushahidi Kesi ya Tundu Lissu

Mahakama Yazuia Kurushwa Mubashara Ushahidi Kesi ya Tundu Lissu Mahakama...

Vyama 17 Vyachukua Fomu Urais wa Zanzibar, CHADEMA & CHAUMMA hawajajitokeza

Vyama 17 Vyachukua Fomu Urais wa Zanzibar Vyama 17 vya...

Related Articles

Popular Categories

Njia Rahisi ya Kuangalia Namba ya NIDA Kwa SMS

Njia Rahisi ya Kuangalia Namba ya NIDA Kwa SMS, Kupata namba ya NIDA kwa njia ya SMS ni rahisi na haraka. Njia hii ni...

Jinsi ya Kupata Mtoto wa Kiume

Jinsi ya Kupata Mtoto wa Kiume, Ni shauku ya kila mzazi kupata Watoto wa Jinsia tofauti katika uzao wao ingawaje Wengi hupata watoto wa...

Jinsi ya Kukopa Muda wa Maongezi Halotel | Menu ya kukopa Salio Halotel

Jinsi ya Kukopa Muda wa Maongezi Halotel, Je Unatumia mtandao wa simu wa halotel na umekwama na hujui hatua ,sifa na vigezo za kupata...