Jeshi la Magereza ni miongoni mwa vyombo muhimu vya ulinzi na usalama nchini Tanzania, lenye jukumu kubwa la kuhakikisha usalama wa jamii kupitia usimamizi wa wafungwa na watuhumiwa walioko chini ya ulinzi wa kisheria.
kwenye makala hii kuna sifa kuu za kujiunga na Jeshi la Magereza Tanzania kwa mwaka 2025, kulingana na tangazo rasmi lililotolewa:
Majukumu Makuu ya Jeshi la Magereza
Jeshi la Magereza Tanzania lina majukumu kadhaa muhimu kwa ustawi wa taifa, ikiwemo:
- Kuwahifadhi wafungwa wa aina zote waliowekwa chini ya ulinzi halali wa kisheria.
- Kuandaa na kutekeleza programu za urekebishaji, ikiwa ni pamoja na kuwafundisha wafungwa ujuzi mbalimbali wa uzalishaji na maisha.
- Kutoa huduma kwa mahabusu kwa kuzingatia misingi ya kisheria na haki za binadamu.
- Kuchangia katika ushauri wa kitaifa kuhusu njia bora za kuzuia na kudhibiti uhalifu.
Kwa njia hii, Jeshi la Magereza husaidia kulinda jamii na kuhakikisha kuwa wafungwa wanapata nafasi ya kubadilika na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi mara baada ya kuachiwa huru.
Sifa za Kujiunga na Jeshi la Magereza Tanzania 2025
Kwa vijana wanaotamani kujiunga na Jeshi la Magereza mwaka 2025, kuna masharti na vigezo rasmi vinavyopaswa kuzingatiwa.
Zifuatazo hapa chini ni sifa kuu zinazohitajika:
1. Lazima uwe Raia wa Tanzania.
2. Unatakiwa kuwa na Kitambulisho cha Uraia au Namba ya NIDA.
3. Usiwahi kuajiriwa katika taasisi yoyote ya Serikali.
4. Umri:
- Wahitimu wa Kidato cha Nne wanatakiwa kuwa na umri kati ya miaka 18 na 24.
- Wenye ujuzi maalum wanatakiwa kuwa na umri kati ya miaka 18 na 28.
5. Lazima uwe na cheti halisi cha kuzaliwa.
6. Urefu:
- Wanaume wanatakiwa kuwa na urefu usiopungua futi 5’7”.
- Wanawake wanatakiwa kuwa na urefu usiopungua futi 5’4”.
7. Uwe na siha njema ya mwili na akili, iliyothibitishwa na daktari wa Serikali.
8. Hutakiwi kuwa umeoa au kuolewa, na wanawake hawatakiwi kuwa wamejifungua.
9. Ili kujiunga na jeshi la magereza hutakiwi kua na alama au michoro yoyote (tattoo) mwilini.
10. Lazima uwe na nidhamu na tabia njema, na usiwe umewahi kupatikana na hatia ya jinai au kufungwa gerezani.
11. Ni lazima uwe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya Askari Magereza na kufanya kazi popote Tanzania Bara.
12. Unatakiwa kuwa tayari kujigharamia katika hatua zote za usaili hadi utakapofika mafunzoni.