Times FM Kutangaza Mubashara Kagame Cup 2025, Kuanzia Tarehe 2 Septemba 

WhatsApp Group Join Now
Telegram Group Join Now

Msimu mpya wa kombe la Kagame (Kagame Cup) unaanza leo, Septemba 2, 2025 kwa mechi mbili kuchezwa kwenye uwanja wa Major General Isamuhyo, Dar es Salaam, mechi hizo zikitarajiwa kutangazwa mubashara na kituo cha radio cha Times FM.

Times FM Kutangaza Mubashara Kagame Cup, Kuanzia Tarehe 2 Septemba 

Times FM Kutangaza Mubashara Kagame Cup 2025, Kuanzia Tarehe 2 Septemba 

Times FM imeingia ubia na Baraza la Soka Afrika Mashariki na Kati ( Cecafa) kutangaza mashindano hayo yanayoanza Septemba 2-15 jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Masoko na mawasiliano wa Cecafa, Andrew Jackson Oryada amesema wameingia ubia na Times FM ambayo itatangaza mubashara mechi zote.

“Tunafuraha kubwa kuwa mshirika na Times FM, kituo pekee cha radio kinachotangaza michezo hapa nchini Tanzania, tunaamini ushirikiano huu utaongeza kwa kiwango kikubwa mwonekano na usikivu wa Mashindano ya CECAFA Kagame Cup 2025,” alisema.

SOMA HII  Ratiba ya Mechi za Simba SC Ligi Kuu Tanzania Bara 2025/2026 NBC Premier League

Alisema kupitia ushirikiano huo, Times FM itatoa matangazo ya kipekee na ya kina ya mashindano ya Kagame Cup, yakiwemo mahojiano na makocha pamoja na manahodha wa timu, matukio ya nyuma ya pazia wakati wa mazoezi, taarifa kutoka vyumba vya kubadilishia, na maudhui ya mchezaji bora wa mechi.

Mashindano haya yatashirikisha timu kutoka Tanzania, Zanzibar, Kenya, Rwanda, Burundi, Somalia, Sudan, Sudan Kusini, Djibouti na Ethiopia.

Mchambuzi wa michezo wa Times FM, Emmanuel Ndalama alisema mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza Septemba 2 hadi 15 yatafuatiliwa moja kwa moja kupitia kituo cha Times FM kama redio mshirika.

“Wasikilizaji kote nchini Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki na Kati wataweza kufuatilia matangazo ya moja kwa moja, mahojiano ya kipekee, uchambuzi wa kina na maoni ya moja kwa moja kutoka viwanjani.

SOMA HII  Ratiba ya Mechi za Yanga SC Ligi Kuu Tanzania Bara 2025/2026 NBC

“Kwa ubia huu, Times FM imeandika historia kama redio pekee ya michezo inayorusha matangazo masaa 24.

Nyota na nahodha wa zamani wa Yanga, Juma Abdul ambaye ni miongoni mwa wachambuzi wa mashindano hayo kupitia radio ya Times FM alisema ni mashindano ambayo yanakwenda kuongeza ushindani na kuonyesha vipaji vipya, akimtolea mfano nyota wa zamani wa timu hiyo, Didier Kavumbagu ambaye alisajiliwa baada ya kuonekana kwenye Kagame Cup.

Bingwa wa msimu huu ataondoka na medali ya dhahabu, kombe na kitita cha dola 30,000, mshindi wa pili medali ya fedha na dola 20,000 wakati mshindi wa tatu atapewa dola 10,000 na medali ya shaba.

SOMA HII  Wasifu CV ya Naby Camara Beki Mpya Simba 2025/26

Hot this week

Nafasi za Kazi Jeshi la Magereza 2025

Jeshi la Magereza limetangaza nafasi mpya za ajira kwa...

Namna Ya Kuangalia Taarifa Za Usajili NIDA | Hatua kwa hatua

Namna Ya Kuangalia Taarifa Za Usajili NIDA, Kuangalia taarifa...

Mfumo wa Maombi ya Ajira kwa Walimu Mtandaoni (OTEAS)

Mwongozo wa Mfumo wa Maombi ya Ajira kwa Walimu...

Orodha ya Vifurushi vya Azam TV na Bei zake – Chagua Kifurushi Kinachokufaa

Azam TV imekuwa sehemu muhimu ya burudani ndani ya...

Sample/Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Jeshi la Magereza

Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Jeshi la...

Wasifu CV ya Neo Maema Kiungo Mpya wa Simba 2025/2026

Klabu ya Simba SC imethibitisha kukamilisha usajili wa kiungo...

Ratiba ya Klabu Bingwa Afrika 2025/2026 Hatua ya Awali

Droo ya mashindano ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF)...

Timu 12 Zitakazoshiriki Mashindano ya CECAFA Kagame Cup 2025

Timu 12 Zitakazoshiriki Mashindano ya CECAFA Kagame Cup 2025 Timu...

Wasifu CV Ya Mohamed Doumbia Kiungo Mpya wa Yanga 2025/2026

Mu Ivory Coast, Mohamed Doumbia (26) ametambulishwa na timu...

Kikosi cha Taifa Stars vs Morocco Leo 22 August 2025 CHAN

Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ itacheza mchezo...

Orodha ya Wafungaji Bora CHAN 2025

Orodha ya Wafungaji Bora CHAN 2025, Michuano ya CHAN...

Wasifu CV Ya Rushine De Reuck Beki Mpya wa Simba 2025/2026

Klabu ya Simba imemtambulisha rasmi beki wa kati, Rushine...

Related Articles

Popular Categories

Njia Rahisi ya Kuangalia Namba ya NIDA Kwa SMS

Njia Rahisi ya Kuangalia Namba ya NIDA Kwa SMS, Kupata namba ya NIDA kwa njia ya SMS ni rahisi na haraka. Njia hii ni...

Jinsi ya Kupata Mtoto wa Kiume

Jinsi ya Kupata Mtoto wa Kiume, Ni shauku ya kila mzazi kupata Watoto wa Jinsia tofauti katika uzao wao ingawaje Wengi hupata watoto wa...

Jinsi ya Kukopa Muda wa Maongezi Halotel | Menu ya kukopa Salio Halotel

Jinsi ya Kukopa Muda wa Maongezi Halotel, Je Unatumia mtandao wa simu wa halotel na umekwama na hujui hatua ,sifa na vigezo za kupata...