Timu 12 Zitakazoshiriki Mashindano ya CECAFA Kagame Cup 2025
Timu 12 ndizo zitakazoshiriki katika Mashindano ya CECAFA Kagame Cup 2025 yanayotarajiwa kufanyika Septemba 2-15 jijini Dar es Salaam, Tanzania huku droo ikipangwa Agosti 26.
Wenyeji Tanzania watawakilishwa na mmoja wa Wawakilishi wao katika Kombe la Shirikisho Afrika Singida Black Stars FC, huku Mogadishu City Club wakiwakilisha Somalia.
Vilabu kama Yanga SC,Simba SC na Aigle Noir CS ya Burundi hazitashiriki kwenye mashindano hayo.
klabu za Mlandege SC (Zanzibar), Kenya Police FC (Kenya), Flambeau du Centre (Burundi), Garde Cotes FC (Djibouti), Ethiopian Coffee SC (Ethiopia), huku Al Hilal Omdurman na Alhly SC Wad Madani wataiwakilisha Sudan, zitashiriki katika kipute hicho.
CECAFA inatarajia kuwa Michuano hiyo itakuwa jukwaa zuri la kuzisaidia timu kujiandaa vyema kabla ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho la CAF.
Mwaka jana timu ya Ligi Kuu ya Zambia, Red Arrows FC iliibuka Mabingwa. Wageni waliwashinda APR FC ya Rwanda katika fainali iliyochezwa kwenye Uwanja wa KMC.